Monday, 15 April 2013

Kwisha! UFARANSA YAPITISHA MUSWADA NDOA ZA JINSIA MOJA, SWEDEN NAKO KIMBILIO LAO

Vuta nikuvute imetokea katika bunge la senate nchini Ufaransa, ambapo mwisho wa siku iliamuliwa kupitisha kwa muswada wa sheria ya kuruhusu ndoa za jinsia moja nchini humo, licha ya upinzani mkali kutoka kwa wabunge wenye msimamo mkali, ikiwamo viongozi wa dini.
Uamuzi huu ambao umepitishwa Ijumaa taehe 12 Aprili 2013 na Ufaransa , taifa lenye asili ya katoliki, umekuja baada ya muda mrefu wa majadiliano, kama ambavyo Rais François Hollande alivyoahidi kwenye uchaguzi mkuu mnamo Aprili mwaka 2012, sera ambayo ilimfanya avune kura nyingi za wafuasi wa ndoa hizo.
Waziri wa Haki, Bi Christian Taubira. © Gouvernement
Mtetezi mkubwa wa muswada huo, waziri wa haki nchini huko, Bi Christian Taubira, amesemema kuwa muswada huo unakuja kutokana na umuhimu wake, hasahasa kwa watoto wanaoishi na wazazi wa jinsia moja, ili wapate haki zao sawa na watoto wa wazazi wa kawaida. na kwa mujibu wa muswada huu, basi wenye ndoa za jinsia moja, watarushusiwa kuasili watoto kwa ajili ya kuwalea.
Tumefanya hivi kwa sababu kuna watoto hawali chakula cha afya, wanakula pipi kwa wingi, na kadha wa kadha, hao pia tunawalinda - wanahitaji hilo. Christian aliwaambia maseneta mara baada ya kupitisha muswada huo, ambao utapitiwa tena February 2014 kwa ajili ya marekebisho.
Kwa upande wake, seneta wa chama cha UMP, Jean-Pierre Raffarin, amesema kuwa bado wataendeleza mpambano kwa kuwa bunge bado lipo, na kilichopo ni kwamba watakuwa wakiongea na wananchi wataobadili mawazo ili kuhakikisha muswada huu unaondolewa na kurejea katika hali ya mwanzo, yaani mume na mke na si vinginevyo.
Mpaka sasa ufaransa imegawanyika kuhusiana na ndoa za jinsia moja, ambapo mnamo January mwaka huu, takriban watu 340,000 waliandamana kupinga ndoa za aina hii, wakisisitiza Baba na Mama kwa familia. Ambapo wiki mbili baadae, kundi la watu takriban 125,000 walijitokeza mtaani kuunga mkono ndoa za namna hiyo.
Nchi ambazo zimeridhia ndoa za jinsia moja mpaka hivi sasa. © CBC
Ulaya ni bara ambalo nchi zake kadhaa zimeruhusu ndoa za namna hii, ambapo kwa watu ambao nchi zao haziruhusu, wamekuwa wakikimbilia huko ili kuonana na kuishi kwa sheria za huko. mfano mmojawapo ni mashoga wawili Waganda, ambao walikimbia nchi yao na kuelekea Sweden ili kuonana kutokana na nchi yao kukataza vitendo vya ushoga na usagaji.
Wadau wa Gospel Kitaa walio nchini Sweden, walifanikiwa kupata tukio hilo kama lilivyofanyika mwezi wa kwanza kwa kamera, na hatimaye mdau Nahshon Kamugisha kuzirusha kwa GK.


Jimmy na Lawrence wakiwa na mashoga wenzao wakati wa sherehe ya 'kuonana'.
Gospelkitaa.com

No comments:

Post a Comment