Monday, 15 April 2013

Gesi ni hatari, Zimamoto wawahi kuokoa.



Gari la zimamoto likiwasili eneo la tukio
Leo asubuhi muda wa saa 3:30 kumetokea mlipuko mkubwa kwenye Glosary ya Kipingu eneo Mtaa wa Sae karibu kabisa na kituo cha Sae. Mlipuko huo wa moto umetokana na jiko la gesi lililokuwa likiwashwa ili kupasha supu na ndipo likalipuka na kuanza kuwaka moto mkali. Moto umezua balaa kubwa kwani kutokana na ukosefu wa vifaa vya tahadhari  vya zima moto na elimu ya majanga watu wakaanza kuzima kwa maji na mchaka lakini ikawa ni kama kuuchochea zaidi. Baada ya kushindika kuzima moto uliokuwa ukiwaka kwenye mtungu wa gesi na kuendelea kusambaa kwenye vyombo vingine ndipo kijana mmoja jasiri maarufu kama KP akajitosa na kuuburuzia nje mtungi uliokuwa ukiwaka moto mkali. Hapo ndipo akawa ameokoa nyumba hiyo yenye maduka manne isiwake moto.
Zimamoto wawahi kuokoa, kinyume na desturi ya zimamoto ya kuchelewa mara wanapoitwa kwenye majanga ya moto kwani waliwasiri mara moja baada ya kupigiwa simu. Zimamoto wamewapongeza wananchi kwa kuweza kuokoka jingo kuwaka moto kwa kuutoa nje mtungi unaowaka moto. Askari wa zimamoto wakauzima moto uliokuwa unaendelea kuwaka kwenye mtungi wa Gesi.
Wasisitiza kutoa taarifa mapema kila mara janga linapotokea kuwakumbusha wananchi kuw ana namba za simu ya kiganjani mbali ya ile ya mezani ili kutoa taaarifa kwa haraka zaidi. Ikumbukwe kuwa mara nyingi zima moto wamekuwa wakilalamikia baadhi ya watu wasio waaminifu wamekuwa waktoa taarifa za uongo kupitia simu ya bure ya 111.
Ushauri wa bure kwa wote wenye majiko ya gesi ni bora wakanunua kifaa cha kuzima moto (Fire Extinguisher) ili watumie kuzima moto mara moto unapolipuka.
Namba za kiganjani za Zimamoto jiji la Mbeya ni
0755 651923
Tazama Picha kutoka eneo la tukio
watu wakushuhudia uzimaji wa mtungi

mtungi umezima

Askari akizima mtungi uliolipuka

 Hata boda boda walikuwepo kujionea wenyewe




 Moto umezimwa tayari kwa safari.
Picha zote na KII

No comments:

Post a Comment