Mwanamke anatembea katika hali ya baridi kali mjini Chicago, Illinois, Jan. 6, 2014.
Wakazi wa mashariki na kusini mwa Marekani wanapambana na baridi kali na
ya hatari kuwahi kutokea baada ya dharuba ya upepo baridi kutoka maeneo
ya kaskazini ya bara la Amerika kupiga na kuenea maeneo ya kati, kusini
na mashariki ya nchi hii.
Hali ya baridi inayoweza kugandisha maji kuwa barafu na theluji katika
muda wa sekunde chache imevunja rekodi ya baridi iliyotokea miaka 10
iliyopita na kufanya hali kuwa hatari kubaki nje na kusababisha maelfu
ya shule na biashara kufungwa.
Kiwango cha baridi kimeshuka chini kwa nyuzi 10 chini ya sifuri kwenye
kipimo cha Celsius hapa Washington DC , Philadelphia na Boston huku
upepo ukiwa ni baridi zaidi na kufanya mtu kuhisi baridi kuwa chini ya
kipmo hicho.
Wakazi wa Marekani wazungumzia baridi kali.
Kushuka sana kwa kiwango cha baridi kumesababisha kuahirishwa kwa maelfu
ya safari za ndege na kuleta mtafaruku barabarani na kwenye njia za
reli. Watabiri wa hali ya hewa wanasema karibu watu milioni 200 wanaweza
kuathiriwa na hali hiyo.
Baadhi ya wahamiaji kutoka Afrika Mashariki wanasema hali hii
inawasababisha kukumbuka nyumbani na hawajawahi kuona kitu kama hichi
ambapo usipojitahadhari unaweza kuwa mgonjwa mara moja au hata kupoteza
vidole vya mikono au miguu ikiwa hujavaa vizuri.
Hali hii ya baridi pia inafikia maeneo ya kusini ambayo ni nadra kupata
baridi kama vile Florida na kusini mwa Texas kawaida maeneo hayo huwa
wanapata baridi ya wastani tu wakati huu wa majira ya baridi.
Maafisa wameamua kufunga mashule ili watoto wabaki salama kutokana na
baridi kali, ambayo inaweza kupelekea vidole kukatika katika dakika
chache kama ngozi ikiachwa wazi.
No comments:
Post a Comment