Saturday, 28 December 2013

Mamia wanasubiri kunyongwa nchini

Share bookmark Print Email Rating
Kutokana na Tanzania kufuata utaratibu wa maadili (moral) katika utawala wake, inaweza kuwa chanzo cha ugumu wa utekelezaji wake. Hukumu ya Kifo hutolewa chini ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act. 1985) ambayo inasisitiza kuwa utekelezaji wa hukumu hiyo ni muhukumiwa kunyongwa na siyo vinginevyo.   Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema 
Na Kelvin Matandiko, Mwananchi

Rais, ndiyo ataamua kusaini ama kutosaini, huwa kuna mambo mengi yanayoangaliwa
Wadhifa wa Urais wa Tanzania umeendelea kujikuta njia panda kila unapofika wakati wa kuidhinisha kutekelezwa kwa adhabu ya kifo kwa waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na mahakama, na suala hilo limekuwa gumu kutekelezwa katika awamu zote nne za uongozi.
Hukumu hiyo ni kama haitekelezeki na pengine mafaili yaliyobeba uamuzi wa mahakama wenye adhabu za vifo, yameendelea kusubiri kusainiwa tangu enzi za uongozi wa awamu ya kwanza wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere na hata sasa Rais Jakaya Kikwete.
Watangulizi wengine wa Rais Kikwete ni Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeongoza Serikali ya Awamu ya Pili na Mzee Benjamin Mkapa, aliyeongoza Serikali ya Awamu ya Tatu. Wote wanatajwa kwamba walikuwa wazito kuidhinisha utekelezaji wa hukumu hiyo ya kuondoa uhai wa mtu.
soma zaidi kwa kubofya http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Mamia-wanasubiri-kunyongwa-nchini/-/1597592/2127326/-/aiaaly/-/index.html

No comments:

Post a Comment