Nimesikitishwa sana kuona makandarasi uchwara kufanya Mbeya kuwa uchochoro wao. Kwani tayari kuna mgogoro usio rasmi wa ujenzi wa soko la Mwanjelwa ambao umesimama kutokana kukosekana pesa wakati huohuo soko lina nyufa kabla halijakamilika. Katika gazeti la Rai la Jumapili tar 23 Nov 2013, Makala yenye kichwa CCM REJEENI KWENYE MISINGI YENU mwandishi ameandika madudu mengi juu ya ujenzi wa soko la Mwanjelwa. Likiwa sakata hilo halijaisha ndio kwanza kamera yangu ikanasa ubovu mwingine katika ujenzi wa taa za barabarani. Ngao zilizojengwa kuzuia taa za barabarani ni mbovu na tayari zimeharibika bila hata ya kugongwa. Nashindwa kuelewa kama nguzo hizo zimejengwa na mkandarasi wa aina gani kwani tayari kumekuwepo kutoaminiwa kwa makandarasi wazawa.
Hebu shuhudia mojawapo ya picha ya ngao zilizovunjika kama zilivyonaswa na kamera yetu kati ya eneo la Ilomba na Sae
Hii ngao imebaki peke yake baada ya taa ya barabarani kung'oka.
Hii ilitengenezwa kingali na mashimo
Hii inakarabatiwa baada ya kuvunjika
Hii imepinda
Imepasuka hovyo kabisa
Hii imekarabatiwa pembeni ya iliyovunjika, sina hakika kama vipimo vimezingatiwa hasa umbali kutoka nguzo ya taa
No comments:
Post a Comment