MWALIMU ni mtu wa muhimu katika jamii yoyote kwa kuwa anabadilisha
maisha ya kila mtu kutoka hatua moja kwenda nyingine. Cha kushanganza
maisha yake ni tofauti na kazi kubwa anayoifanya. Pia wanapata
changamoto nyingi katika utendaji kazi wao… wengine wanajikuta
wakivikimbia vituo vyao vya kazi kutokana na mazingira magumu
wanayofanyia kazi.
Jambo la kusikitisha walimu wanafikia hatua ya kutembea kilomita kubwa kutoka majumbani kwao kwenda kwenye vituo vyao vya kazi hali ambayo haiwezi kuleta matokeo mazuri ya elimu nchini.
Mwalimu anatembea kila siku kilometa 10 kwenda na kurudi kutoka shuleni, anafika amechoka na hana hamu ya kufundisha hivyo anafundisha chini ya kiwango kinachotakiwa.
Licha ya Serikali kujitahidi kuajiri walimu wengi kwenye vituo mbalimbali karibu mikoa yote ya Tanzania, bado imesahau kuwa baada ya kutoa ajira walimu wanaenda kukaa katika mazingira gani.
Idadi kubwa ya walimu wanapelekwa maeneo ya vijijini kutokana na uhaba wa walimu katika maeneo hayo, lakini huduma za kukidhi mahitaji yao bado ni hafifu.
Inasikitisha kuwaona walimu ambao ni mhimili mkubwa katika jamii wanalala jikoni kwa miaka mitatu huku wafanyakazi wengine wakiwa wanatembea zaidi ya kilomita kumi, jambo hili linasikitisha na linatia aibu kwa Serikali yetu.
Kuhusu walimu wanaotoroka kazini na kujiunga na vyuo vya elimu ya juu pasipo ridhaa ya mwajiri, tatizo hili linaathiri zaidi mikoa iliyopo Kanda ya Ziwa na Kaskazini, ambayo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu ambapo chanzo kikubwa ni mazingira mabaya ya kufanyia kazi.
Taratibu za kuyarekebisha maisha ya walimu yatasaidia kupunguza utorokaji wa walimu katika maeneo mbalimbali hapa ikiwemo vijijini ambapo matatizo yanakuwa mengi kuliko wale wa mjini.
Walimu wengi hukimbilia mjini ili kukwepa matatizo ya vijijini ambapo baadhi yao wanajikuta wakiishi kwenye nyumba za udongo na kuamua kuachana na kazi ya ualimu na kujihusisha na biashara nyingine.
Kutokana na hali kuwa tete Serikali ilipanga kuwachukulia hatua watumishi wake zaidi 800 waliotoroka kazini na kujiunga na vyuo vya elimu ya juu bila idhini ya mwajiri.
Jumla ya walimu 26,537 wameajiriwa serikalini kwa mwaka wa fedha 2012/2013, walimu wa ngazi ya cheti walioajiriwa ni 13,568.
Kati yao walimu 13,527 wamepangwa kufanya kazi katika shule za msingi zilizopo kwenye halmashauri na walimu 41 wamepangwa katika shule za msingi za mazoezi zilizo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Jumla ya walimu wa sekondari na vyuo vya ualimu walioajiriwa ni 12,973 wakiwemo walimu wa Shahada 8,887 na Stashahada 4,086, lakini swali la kujuuliza maeneo waliyopangiwa yanakidhi viwango?
Idadi ya walimu walioajiriwa mwaka 2012/2013 imeongezeka kwa asilimia 11 sawa na walimu 2,630 ikilinganishwa na walimu 23,907 walioajiriwa mwaka uliopita 2011.
Walimu wapya wanakuwa na shauku kubwa ya kuanza kazi, lakini baada ya kuripoti kwenye vituo vyao vya kufanyia kazi na kukuta mazingira si mazuri baadhi yao wanaamua kuondoka baada ya wiki tatu au mwezi mmoja.
Baada ya Serikali kutilia shaka matokeo hayo Baraza la Mitihani Tanzania (BAMITA) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wameamua kurudia kusahihisha lakini matokeo hayajabadilika kwa asilimia kubwa sio siri ufaulu si nzuri kama inavyotakiwa.
Licha ya Serikali kujitahidi kuwaajiri walimu kwa wingi kila mwaka lakini hali bado ni mbaya hasa maeneo ya vijijini ambapo unaweza kuikuta shule ina jumla ya wanafunzi mia 400 lakini wanafundishwa na walimu wawili au watatu hali ambayo haiwezi kuleta matokeo mazuri.
Walimu hawawezi kufanya kazi zao kwa ufanisi ulio juu huku wakiwa wanalala jikoni kwa miaka mitatu na wengine kutembea kwa kilomita kumi,kitu ambacho hakiwezekani.
Wanafunzi wa sasa wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika lakini mwanafunzi huyo anafaulu kwenda kidato cha kwanza,kwa hali hii tusitegemee kupata matokeo mazuri na viongozi wazuri wa baadaye.
Chanzo; Mtanzania.co.tz

No comments:
Post a Comment