m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Sunday, 12 January 2014

JAMANI MANABII NA MITUME KWELI HAYA NDIO MAOMBI KULA MANYASI? MWE

Mdada akila majani ambayo huduma hiyo wanasema ni chakula kutoka mbinguni mwe!
Kuna mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu huduma za watumishi mbalimbali, moja wapo ni hii huduma iitwayo Rabboni Centre ministries iliyopo Pretoria nchini Afrika ya kusini, huduma hii iliyochini ya mwanzilishi wake mwalimu ,mchungaji na nabii Daniel Lesego ilianza mwaka 2002. Ni huduma ambayo kwa watu wasioabudu hapo huitilia mashaka kutokana na mwenendo wake.

Kwasasa wapo kwenye mfungo ambao watu hufika kanisani na hatimaye wanaishia kula majani yaliyopo nje ya kanisa hilo akisema kwamba Roho Mtakatifu huongoza mtu kula chochote huku ikidaiwa kuwa manyasi hayo ni chakula kutoka mbinguni.

Inaelezwa kwamba mara baada ya maombi waumini wengi huanza kutapika jambo ambalo kanisani hapo huashiria kwamba mtu amejazwa Roho Mtakatifu.

Lakini kama haitoshi nabii Lesego hufanya maombi huku amewakanyaga watu. Huduma hii imekuwa gumzo nchini humo na nchi jirani kwa jinsi mambo yao yanavyokwenda.

Mnasemaje watumishi kuhusu jambo hili? mwe kula manyasi kweli? mma!

Hapa nabii huyo akikanyaga watu kama njia ya mafundisho yake.
Haa!! angalia jamani, sasa ng'ombe watakula nini jamani???
Mungu tufunulie macho ya rohoni kuyajua mambo haya kama ni wewe au sisi kha!
Hajamaliza bado.
Baada ya manyasi ni mwendo wa kutapika sasa







Picha ya juu na hii huyu ndio nabii Lesego Daniel mwenye maono na huduma hii.
Watu wanajaa kwenye huduma.
Mwe! kama uti wa mgongo shida hii dawa 
Maombi yanaendelea.
Waumini wakikaribisha mwaka mpya.
Nabii anafundisha huku skuna yake imekanyaga mtu, sijui 

Tembelea TOVUTI YAO  Picha zote kwa hisani ya ukurasa wao wa Facebook.
Chanzo : gospelkitaa.blogspot.com

Saturday, 11 January 2014

RIPOTI YAONYESHA WAKRISTO WA TANZANIA HATARINI

Tanzania imeshika nafasi ya 49 kati ya nchi 50 ambazo Shirika la Open Doors la Marekani katika ripoti yake ya mwaka "2014 Watch List" imesema ndio nchi hatari zaidi duniani kwa wakristo kuishi. Katika ripoti hiyo Open doors wameiweka Tanzania katika kundi ambalo wakristo huishi kwa wasiwasi huku pia likitoa idadi ya nchi 10 ambazo ni hatari zaidi duniani kuwa Mkristo. Open doors hujishughulisha na kusaidia wakristo waliopo vifungoni wakiwa katika hatari ya kuuwawa kutokana na kutetea ama kuhubiri injili ya Yesu Kristo.
Katika orodha iliyotoa, shirika hilo limeonyesha nchi ambazo wakristo wanaishi kwa kujificha, manyanyaso, kutekwa lakini pia wakiwa katika hatari ya kuuwawa na serikali za nchi hizo ama vikundi hatari vya dini vya watu wenye msimamo mkali wa dini.
Hii ni listi ya nchi hatari zaidi duniani kwa wakristo kuishi, ambao hadi Tanzania kushika '50 bora', basi hakika hilo ni jambo la kuombea kwa nguvu zote, na kama hufahamu, Baraza la Makanisa ya Kipentekoste nchini limeshatangaza maombi ya kufunga na kuomba kwa siku 40 kuanzia Januari 6, hili ni mojawapo ya jambo linalostahili kushughulikiwa.

Taarifa za nchi tano duniani ambazo ni hatari zaidi kwa wakristo kuishi ni kama ifuatavyo;
1. NORTH KOREA/KOREA KASKAZINI
  • Ni kosa la jinai kuwa mkristo au kushiriki katika shughuli za za Kikristo
  • Katika vizazi vitatu mpaka sasa mmoja kati ya wanafamilia kuna uwezekano wamefungwa kwa kosa la kumiliki Biblia.
  • Takribani wakristo 70,000 wapo gerezani wakitumikishwa kwa shughuli mbalimbali
2. SOMALIA
  • Wakristo wanahusishwa kushirikiana na upande wa mataifa ya kikoloni yenye nguvu ya Ulaya
  • Imependekezwa adhabu ya lifo kea mtu kuwa mkristo
  • Kutokana na ukosefu wa serikali makini fujo zinazoletwa na vikundi vinavyopinga ukristo vinapewa nguvu na majeshi ya nchi.
3. SYRIA
  • Makumi elfu wamekuwa wakihama makazi kutokana na vitisho na vurugu
  • Takribani 50-60,000 ya wakristo katika mji wa Homs wameondolewa
  • Makanisa mengi yamelipuliwa.
4. IRAQ/Iraki
  • Idadi ya wakristo wanaoishi kwenye mateso inazidi kuongezeka toka vita ya kwanza ya Juba mwaka 1990
  • Ongezeko la vitendo vya utekaji nyara, vitisho na mauaji tokea vita ya Gulf mwaka 2003.
  • Asilimia 25 tu ndio wakristo sawa na idadi ya mwaka 1990
5. AFGHANISTAN
  • Serikali imetoa vitisho vya adhabu ya kifo kwa yeyote atakayeacha Uislamu
  • Kuna wakristo 1,200 nchi nzima
  • Hakuna makanisa.

Imeandikwa awali na Christian Post, ukitaka kuona idadi kamili ya nchi 50 duniani ambako wakristo wapo hatarini bonyeza hapa.
CHANZO: gospelkitaa.blogspot.com

Friday, 10 January 2014

Mpango kwa Vijana na Mustakabali wa Ajira



Wapenzi wangu leo nipo tena ili kukushirikisha katika habari zetu KII. Kama ujuavyo moto wetu ni “habari ni Maisha” kumbe ukikosa habari huna maisha na ukipata habari njema utakuwa na maisha mema na ukipata habari mbaya ni matokeo ya maisha mabaya. Kilichopo mezani leo ni juu ya vijana wenzangu na mpango unaopaswa kuwasaidia vijana.
Ndugu zangu sina mpango wowote unaoweza kuwasaidia vijana lakini nafikiri kwamba ni stahiki sana kuwa na mpango huo kama tunalitakia mema Taifa letu. Kumekuwa na ongezeko la vijana nchini, katika ongezeko hilo kuna kundi kubwa la vijana wasio na elimu wala ajira na kundi la pili ni lile lililo katika mfumo wa elimu na hata kupata elimu lakini likiwa na wasiwasi wa ajira. Ongezeko hilo ndio linalonitia wasiwasi na hatima ya Taifa letu hivyo kunisukuma kuandika makala haya.
Kabla sijaendelea naomba nigusie uhalifu katika majiji makubwa na yanayoongoza kwa uhalifu duniani, nazungumzia Paris –ufaransa Rio De Jeneiro- Brazil na Johannesburg- Afrika kusini. Ndio majiji hatari zaidi duniani kwa uhalifu lakini swali la kujiuliza ni nani wanaofanya uhalifu huo? Na kwanini? Kwa haraka utagundua kuwa majiji hayo ndio yale yenye vijana wengi waliokosa ajira. Katika majiji hayo matatu utabaini zaidi kuwa majiji mawili ni yale yenye mgogoro wa ubaguzi wa rangi. Sitaki kuzungumzia sana ubaguzi wa rangi bali nataka kugusia ubaguzi na mipango mibovu kwa vijana katika maendeleo ya Taifa lolote duniani Tanzania ikiwa mfano. Afrika kusini ilikumbwa na ubaguzi wa rangi na katika ubaguzi huo uligusa pia elimu na ajira pasipo kujali athari itakayopata baadaye. Hali kadhalika Paris ilikumbwa na wahamiaji haramu wa Afrika kaskazini hasa kutoka nchi za Algeria na makoloni yake kama Senegal. Wahamiaji wakaingia  nchini ufaransa na wenyewe wakawaadhibu si tu kuwafukuza bali hata waliobaki kwa kuwabagua kama wasio na haki nchini humo. Athari yake ndio yanayowapata sasa kwani wale vijana waliobaguliwa na kunyimwa elimu au ajira sasa wamegeuka kuwa wahalifu kama njia yao ya kujikimu na maisha.
Unapoamua kuwa mbaguzi lazima ujitenge kabisa jamii ile unayoibagua na ikiwa umeamua kuishi nayo ni lazima ukatae ubaguzi kwa gharama zote, huwezi kumbagua siku zote mtu unayeishi naye mahali pamoja.
Nchi yetu sasa ina ongezeko kubwa la vijana wasomi na wasio wasomi bila kuwepo na mipango madhubuti  ya kuwasaidia kukabili changamoto ya ajira. Watawala hujisahau sana kuhusu vijana kwani huona wao na familia zao wako salama hakuna tatizo lolote kwani hata ajira zimekuwa kwa kibendera. Hakuna mipango  ya makusudi ya kuwasaidia vijana katika ajira na ukizingatia mfumo wetu wa elimu unamuandaa kijana kuwa afisa wa kukaa ofisini tu, mfumo wa elimu ya kikoloni ili wakoloni kujipatia maofisa wachache katika ofisi zao kuendelea kuwatawala waafrika. Kuna haja ya kuwepo kwa mipango ya namna vijana wanavyoweza kutengeneza ajira mbali ya kung’ang’ania zile za serikali na mashirika kwani tayari kuna wasomi wengi kwa ngazi ya sekondari, astashahada, stashahada hadi shahada wasio na ajira na bado wana matumaini ya kuajiriwa. Wana matumaini makubwa kila watazamapo vyeti vyao lakini ukweli ni kwamba hakuna ajira nchi hii tupilia mbali zile chache ziwatoshao wenyewe. Nchi isiyo na viwanda, isiyo na miundombinu ya afya na elimu haiwezi kuwa na ajira za kutosha kwani wataalamu ambao wangeajiriwa kwenye hospitali, shule, vyuo, migodini na viwandani itawalazimu kubaki wakirandaranda mitaaani wakiwa na matumaini ya ajira ilhali hakuna ajira.
Mpango niutakao ni kuwabadili vijana wasifikiri juu ya njia moja ya ajira yaani kutegemea kuajiriwa badala yake kujiaajiri, wafunzwe kwamba ajira ni pamoja na kujiajiri  na hata kutengeneza ajira kwa ajira kwa ajiri ya wengine. Serikali inapaswa kufanya mambo mawili muhimu kubadili mtazamo wa vijana katika ajira na pili ni kuwasafishia njia ya kujiajiri. Binafsi sioni njia bora ya kujiajiri katika nchi zaidi ya viwanda na kilimo ndio nafasi zinazopaswa kupewa kipaumbele. Nchi ya Tanzania bado haijawa ya kiviwanda na wala sioni kama ni nchi ya kilimo inababaika tu lakini tunaweza kuleta mageuzi na mageuzi yoyote huletwa na vijana hata uhuru wa Afrika uliletwa na vijana machachari akina Kwame Nkrumah, Mwl. J.K Nyerere, komredi R. Mugabe na wengineo. Tugeukie viwanda kwani nchi yetu ina matumizi makubwa kabisa ya bidhaa za viwandani lakini ajabu ni kwamba asilimia kubwa ya bidhaa hutoka nje ya nchi. Kama ni elimu tayari tunayo japo viwanda vingine havihitaji elimu, kwani ni elimu gani inahitajika ili kutengeneza vijiti vya meno (Toothstick), Kalamu, rula, chaki n.k mbona navyo vyatoka nje? Ni dhahiri kuwa kama vingetengenezwa nchini tungetengeneza ajira kwa vijana wengi kabisa. Inashangaza kuona nchi bado inategemea bidhaa ndogondogo za nyumbani kama sabuni, sukari, chumvi, kutoka nje ya nchi na watanzania wakiona fahari kutumia bidhaa za nje kuliko za ndani. Binafsi nimekuwa nikitoa semina za ujasiriamali ninapopata nafasi ya kufanya hivyo katika pitapita yangu katika mitandao ni mebaini kuna mitambo ya hadi milioni 8 na hata ya chini ya hapo inayoweza kuchonga bidhaa ndogondogo kama mishumaa, vijiti vya meno na kutengeneza chaki ni mitambo rahisi isiyohitaji elimu kubwa. Mbali ya hivyo serikali iliyoweza kuwashawishi wenye viwanda kutoka nje kama kiwanda cha Nation kilichokuwa kinazalisha betri na redio za nation inashindwaje leo kuwashawishi Wajapan, wachina na wahindi kuleta viwanda vyao nchini ili tusiendelee kuagiza bidhaa za kielekroniki kama redio, ngamizi, simu na magari wakati sisi ni wateja wao wakubwa? Sijui wizara inayohusika na viwanda inafanya nini kuhusu hili na wizara inayohusika na ajira inaishauri nini wizara ya viwanda? Kama hakutakuwa na hatua za makusudi kuongeza viwanda vidogo na vya kati ajira itaendelea kuwa tatizo kubwa na mfumuko wa bei utakuwa donda ndugu katika nchi yetu kwani tumekuwa na matumizi makubwa ya fedha za kigeni kuliko uzalishaji.
Katika kilimo bado hatujaamua kukifanya kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu na hatimaye kutengeneza ajira. Kwetu kilimo imebakia kuwa sekta ya walalahoi na watu waliokosa elimu, fikra potofu kabisa. Hebu tazama pamoja na kuwepo kwa mapori mengi bado nchi imekuwa na tatizo kubwa la chakula katika mikoa ya Shinyanga, Singida na Dodoma. Maana yake mahitaji ya chakula yamekuwa makubwa kuliko uzalishaji wakati huohuo kukiwa na tatizo la ajira. Watu hawana la kufanya wakati mapori yanakaa bure na mahitaji ya chakula ni makubwa. Ni ajira ngapi tupata kama tukamua kuzalisha chakula cha kutosheleza mahitaji yetu potelea mbali kuzalisha kwa ajili ya kuuza nje ya nchi ambako pia kuna mahitaji makubwa ya chakula? Ajabu zaidi hata matunda yanatoka Afrika ya Kusini kwa mfano Tufaha maarufu kama apple huagizwa kutoka Afrika ya kusini ingawa yanastawi maeneo ya baridi kama Iringa na Njombe. Kuna haja gani ya kunywa maziwa ya Kenya ili hali tuna mamilioni ya ng’ombe nchini? Nina maswali mengi yakisubiri majibu.

China tuionayo leo hatukuwa na tofauti sana tulipokuwa tunapata uhuru,  imestawi sana baada kujihakikishia kwanza soko la ndani la bidhaa zake yaani wananchi wake yenyewe, wakafanya uzalishalishaji mkubwa ndipo kutanua uchumi wake na kuweza kushindana na mataifa makubwa kiuchumi. Nasi tuna soko letu la ndani kwani watu milioni arobaini na uchee si haba. Tukizalisha kwa ajili yetu tu tutaiimarisha shilingi yetu na hatimaye kuwa na uchumi unaostawi lakini vijana wakipata utulivu kwa ajira kemkem.

Tazama utengenezaji wa vijiti vya meno
 Picha za mashine rahisi za kutengeneza vijiti na mishumaa


Lazima uandaliwe mpango kwa ajili ya vijana na kupata mustakabali wa  baadaye wa kwao wenyewe vijana na Taifa letu. Kama haitafanyika hivyo nchi hii haiitakuwa salama tena kwani wasionacho watapopoteza matumaini utakuwa mwanzo wa uhalifu mkubwa kwa walionacho. Hatuna tofauti na nchi za Ufaransa na Afrika Kusini kwani hata elimu yetu ni ya kibaguzi kwa sehemu kwani  wenye nacho wanapata elimu bora kuliko wasionacho na katika ajira vivyo hivyo.
Hata hivyo ninatoa rai kwa vijana kuwa tayari kwa ajili ya ajira yoyote yenye kuingiza kipato wawe tayari kutumia uwezo wao wote kubuni ajira ili kuleta mageuzi kama tukitaka ajira za serikali tu nchi yetu itaangamia na katika kuangamia huko athari kubwa ni kwa makabwela kama siye.
Wako katika safari                                                   
Ndg. Peter Kapagi                                                                                                    09.01.2014
                                                                                                                                    Mbeya

Uganda,Rwanda, Kenya wakubaliana himaya moja ya ulinzi

Mawaziri wa ulinzi na wa mambo ya ndani kutoka nchi za Uganda,Rwanda na Kenya wametia saini makubaliano kuweka himaya moja ya ulinzi miongoni mwa nchi hizo.
Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki-kutoka kushoto: Uhuru Kenyatta, Yoweri Museveni na Paul Kagame Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki-kutoka kushoto: Uhuru Kenyatta, Yoweri Museveni na Paul Kagame
Hii ni mara ya kwanza kuwepo kwa mkataba huo na hii ina maana nchi moja ikipata matatizo ya usalama nchi nyingine zitakuwa na uhuru wa kuingilia kati na kusaidia. Kikao cha mawaziri hao kilitanguliwa na kile cha wakuu wa majeshi na polisi kutoka nchi hizo ambacho pia kilitathmini changamoto za kiusalama kwenye eneo hilo na jinsi ya kuimarisha ushirikiano miongoni mwa mataifa hayo. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Sylivanus Karemera
Mhariri: Mohammed Khelef
chanzo:dw.de

Wamarekani wapambana na baridi kali kuwahi kutokea.


  • Mwanamke anatembea katika hali ya baridi kali mjini Chicago, Illinois, Jan. 6, 2014.
    Wakazi wa mashariki na kusini mwa Marekani wanapambana na baridi kali na ya hatari kuwahi kutokea baada ya dharuba ya upepo baridi kutoka maeneo ya kaskazini ya bara la Amerika kupiga na kuenea maeneo ya kati, kusini na mashariki ya nchi hii.
    Hali ya baridi inayoweza kugandisha maji kuwa barafu na theluji katika muda wa sekunde chache imevunja rekodi ya baridi iliyotokea miaka 10 iliyopita na kufanya hali kuwa hatari kubaki nje na kusababisha maelfu ya shule na biashara kufungwa.
    Kiwango cha baridi kimeshuka chini kwa nyuzi 10 chini ya sifuri kwenye kipimo cha Celsius hapa Washington DC , Philadelphia na Boston huku upepo ukiwa ni baridi zaidi na kufanya mtu kuhisi baridi kuwa chini ya kipmo hicho.
    Wakazi wa Marekani wazungumzia baridi kali.

    Kushuka sana kwa kiwango cha baridi kumesababisha kuahirishwa kwa maelfu ya safari za ndege na kuleta mtafaruku barabarani na kwenye njia za reli. Watabiri wa hali ya hewa wanasema karibu watu milioni 200 wanaweza kuathiriwa na hali hiyo.

    Baadhi ya wahamiaji kutoka Afrika Mashariki wanasema hali hii inawasababisha kukumbuka nyumbani na hawajawahi kuona kitu kama hichi ambapo usipojitahadhari unaweza kuwa mgonjwa mara moja au hata kupoteza vidole vya mikono au miguu ikiwa hujavaa vizuri.

    Hali hii ya baridi pia inafikia maeneo ya kusini ambayo ni nadra kupata baridi kama vile Florida na kusini mwa Texas kawaida maeneo hayo huwa wanapata baridi ya wastani  tu wakati huu wa majira ya baridi.
    Maafisa wameamua kufunga mashule ili watoto wabaki salama kutokana na baridi kali, ambayo inaweza kupelekea vidole kukatika katika dakika chache kama ngozi ikiachwa wazi. 
    Chanzo: voaswahili.com

Thursday, 9 January 2014

Al Shabaab yaharamisha Internet


Shabaa limetoa makataa ya siku kumi na tano kwa wanaotoa huduma za internet kuzifunga
Wanamgambo wa Al Shabaab wenye uhusiano na Al-Qaeda, wamesema kuwa wamepiga marufuku raia wanaoishi katika maeneo wanayodhibiti kutumia internet.
Wapiganaji hao wametoa makataa ya siku 15 kwa kampuni zote zinazotoa huduma ya internet kufunga biashara zao.
"kampuni yoyote au mtu yeyote atakayepatikana akipuuza onyo hilo atajulikana kama mtu anayewafanyia kazi maadui zetu, na ataadhibiwa kulingana na sheria za ziisilamu,'' ilisema taarifa ya kundi hilo ambayo ilitumwa kwenye mitandao yake.
Wanamgambo hao hutumia sheria kali za kiisilamu katika maeneo wanayotawala na kuwakamata watu mara kwa mara kwa tuhuma za kufanya ujasusi.
Internet hutumiwa sana nchini Somalia, taifa ambalo limekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miongo miwili, huku kundi hilo likionekana kuwa kikwazo kikubwa kwa amani.
Kundi la al Shabaab zamani lilikuwa likitawala katika sehemu kubwa za Kusini mwa Somalia na Kati, lakini likaondoa wapiganaji wake baada ya kushindwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika wanaopambana nao.
Majeshi ya Afrika ikiwemo wanajeshi kutoka Uganda, Burundi na Kenya, tangu hapo wamedhibiti sehemu kadhaa kutoka kwa wapiganaji hao.
Lakini mashambulizi ya kuvizia yanayofanywa na kundi hilo dhidi ya maslahi ya majeshi ya serikali na yale ya kigeni, yameondoa matumaini ya kunusuru taifa hilo kutokana na vita vya miaka mingi.
chanzo: dw.de

Monday, 6 January 2014

Chadema yawatimua Dk Kitila, Mwigamba


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akiandaa nyaraka za ushahidi dhidi ya viongozi waliofukuzwa kwenye chama hicho juzi, kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu. Picha na Fidelis Felix 
Na Fidelis Butahe na George Njogopa, Mwananchi

Posted  Jumatatu,Januari6  2014  saa 8:9 AM
Kwa ufupi
  • Yasema waraka wao wa mabadiliko ulikuwa na nia ya kukimaliza chama na viongozi wake wa juu

Dar es Salaam. Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imewafukuza uanachama, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo.
“Tumewavua uanachama kutokana na makosa ya kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013,” alisema Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa mbele ya waandishi wa habari.
Wakati hayo yakifanyika, imeelezwa kuwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe ataendelea na  uanachama na ubunge kwa sababu ya mahakama, siyo kwa matakwa ya chama hicho.
Zitto ambaye alitajwa kuwa mhusika mkuu katika waraka huo amefungua kesi akiomba Mahakama Kuu izuie uanachama wake kujadiliwa hadi rufani yake itakaposikilizwa na Baraza Kuu la chama.  Hatima ya maombi hayo itajulikana leo.
Maamuzi ya kikao
Akitangaza uamuzi wa kikao cha dharura cha Kamati Kuu kilichokutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam jana, Dk Slaa alisema, “Kuhusu Zitto Kamati Kuu haikujadili wala kuamua juu ya mashtaka dhidi yake.”
Huku akiyataja makosa 11 ya Zitto, Mwigamba na Dk Kitila yaliyotokana na waraka huo, Dk Slaa alisema, “Baada ya kumhoji Dk Mkumbo alikiri wazi kuwa Zitto alikuwa akiujua waraka huu ambao ulilenga kukiuka chama, kutengeneza tuhuma dhidi yangu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.”
Katika mkutano huo Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu alisema Zitto ataendelea kuwa mwanachama wa Chadema na mbunge kwa sababu ya  mahakama na siyo matakwa ya Chadema.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mwigamba na Dk Kitila, Novemba 22 mwaka jana walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu baada ya kukamatwa kwa waraka huo.
Waraka huo ulioandaliwa na Mwigamba na Dk Kitila, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho, huku Zitto akipendekezwa kuwania nafasi ya uenyekiti.
Utetezi wa watuhumiwa
Katika ufafanuzi wake kuhusu utetezi wa watuhumiwa, Dk Slaa alisema, “Dk Kitila pekee, ndiye alikuja kuhojiwa na Kamati Kuu iliyokutana Januari 3 hadi 4 na kwamba alikubali kuandaa waraka lakini alikataa kwa kuwa ulikiuka katiba na kanuni za chama. Pia alikataa kumtaja kwa jina mwandishi mwingine wa waraka huo anayetajwa kwa jina la M2.”
Soma zaidi http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/Chadema-yawatimua-Dk-Kitila--Mwigamba/-/1597332/2135732/-/k2po63/-/index.html

Friday, 3 January 2014

Hali ya Ariel Sharon yazorota zaidi

Sharon alisifika zaidi kwa msimamo wake mkali wa kisiasa
Hali ya kiafya ya waziri mkuu wa zamani wa Israel, Ariel Sharon - ambaye amekuwa katika hali mahututi, inaendelea kuzorota zaidi.
Inaarifiwa kwamba maisha yake yamo hatarini.
Madaktari wanasema kuwa Sharon mwenye umri wa miaka , 85, anakabiliwa na matatizo ya afya ya viongo vyake vya mwili ikiwemo Figo zake na kwamba vinaanza kuonekana kutofanya kazi vyema.
Hata hivyo madaktari hawakutoa taarifa zaidi kuhusu afya ya Sharon.
Alichukua wadhifa wa waziri mkuu mwaka 2001 na kuugua kiharusi mwaka 2005 na alisifika sana kwa msimamo wake mkali kuhusu hali ya kisiasa kati ya taifa hilo na utawala wa Palestina.
Baada ya kupatwa na kiharusi kingine mwaka 2006, Sharon akapotewa na fahamu na amekuwa kwenye mashine ya kusaidia moyo wake kuendelea kupiga tangu hapo.
Sharon alikuwa mmoja wa wanasiasa mashuhuri wenye utata katika siasa za Israel.
Chanzo; bbcswahili.com

Thursday, 2 January 2014

MAHARI YASABABISHA NDOA ISIFUNGWE

Bwana Harusi Fadhili Mahenge akiwa ndani ya Suti akisubiri kufungishwa ndoa 
Bi Harusi Naomi Ngoje akiwa amejilalia chumbani akisubiri hatima ya Wazazi ndipo ajiandae kwenda kanisani tayari kwa kufunga ndoa na mchumba wake waliodumu kwa miezi saba.
Bwana harusi akiwa na mpambe wake kanisani wakimsubiri bibi Harusi
Askofu Kenani Mpalala akiwa katika picha ya pomaja na Bwana Harusi na mpambe wake muda mfupi baada ya kuwasili kanisani
Askofu Keenan Mpalala wa kanisa la Free Pentecost Church of Tanzania akionesha tangazo la Ndoa
Baadhi ya ndugu wa mwanamke wakiwa katika kikao na kuendelea na msimamo wao kuwa mahali lazima imalize ndipo wamtoe binti yao
Jamaa wameshika vichwa hali haieleweki


Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Ndugu Benson Mbwana(aliyevalia shati rangi ya Zambarau) akionyesha ratiba ya sherehe.
Baadhi ya akina mama wakiangalia ratiba ya harusi
Kanisani
Baadhi ya waumini na majirani wakisubiri kanisani



KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Familia moja ya Makunguru  Mtaa wa Ilolo Jijini Mbeya imesababisha sintofahamu dhidi ya Familia nyingine baada ya kumkatalia binti yao kuolewa kwa madai ya waoaji kutokamilisha Mahari waliyokuwa wamepangiwa.

Tukio hilo la aina yake limetokea leo ambapo Bwana harusi aliyefahamika kwa jina la Fadhili Mahenge(28) Mkazi wa Songea aliyekuwa amuoe Naomi Ngoje na harusi yao kufungwa katika kanisa la Free Pentecoste Church Of Tanzania(FPCT) lililopo Makunguru Jijini hapa kushindwa kufungwa baada ya wazazi wa Bibi harusi kuzuia ndoa hiyo hadi Mahari itakapokamilika.

Wakizungumzia tukio hilo Nyumbani kwa Familia ya Bibi Harusi, Mjomba wa Bibi Harusi Dickson Ngoje amesema tatizo la wao kugomea ndoa hiyo ni kutaka waoaji kutimiza masharti waliokuwa wamekubaliana awali ambayo hadi siku ya mwisho familia hiyo haijatekeleza.

Amesema siku ya kwanza waoaji walifika Nyumbani kwa Mzee Ngoje na kujitambulisha ambapo walipangiwa taratibu za mahari kwa mujibu wa Mila kuwa watatakiwa kutoa Blanket 2, Mashuka mawili, Mkaja(200,000), mbuzi 4, Majembe 4, Ng’ombe Jike 2 na Ngo’mbe Dume 1 pamoja na fedha taslimu Shilingi Laki 3.

Amesema baada ya Familia hiyo ya Waoaji ambao ni Ukoo wa Mahenge kupangiwa vitu hivyo waliondoka na kuahidi kurudi siku nyingine kwa ajili kukamilisha vitu walivyopangiwa ambapo walirudi Septemba 11, Mwaka huu wakiongozwa na Mshenga aliyejulikana kwa jina moja la Mzee Katete wakiwa na Blanketi 2, Mashuka mawili pamoja na Fedha shilingi 10,000/= ambazo walizipokea na kuwaambia hawawezi kuzungumza chochote juu ya Ndoa.

Mjomba huyo anaongeza kuwa baada ya wiki mbili familia hiyo ilirudi na kukuta Nyumbani kuna ukoo mzima wakiwa na Shilingi 200,000/= ndipo walipoambiwa walipe kiingilio shilingi 100,000/= ndiyo wanaweza kupokelewa nyumbani jambo ambalo walilitekeleza kisha kulipa fedha walizokuwa nazo kama Mkaja na kuomba wapewe kibali cha kuandikisha ndoa na taratibu za kumalizia vilivyobaki zikiendelea.

Anasema tangu hapo Ndoa ilianza kutangazwa Disemba 8 na kuisha Disemba 22, Mwaka huu baada ya kutangazwa mara tatu huku tangazo likiashiria ndoa kufungwa tarehe 28/12/2013 ambapo wazazi wakiahidi kumalizia Mahari iliyobaki kabla ya siku ya kufunga ndoa.

Akizungumzia kwa kirefu kashishe hiyo, Mjomba huyo anasema baada ya wazazi wa Mwanaume kusisitiza kumaliza kila kitu hadi ifikapo Disemba 23, Mwaka huu na wao walijikusanya na kupanga taratibu za sherehe hususani ya kumwaga binti yao(Send Off) ambayo ilifanyika Disemba 24, Mwaka huu.

Aidha baadhi ya ndugu wameongeza kuwa familia hiyo haioneshi uaminifu wa kumalizia Mahari hiyo kutokana na ahadi zisizotekelezeka walizotoa tangu kipindi cha nyuma na kuongeza kuwa hata kwenye sherehe ya kumwaga binti yao walifika baadhi ya ndugu wakiwa na Zawadi tofauti na taratibu zinavyotaka.

Wamesema kwa mujibu wa taratibu za Sherehe za SendOff upande wa Mwanaume unatakiwa kuleta zawadi ambazo ni  nguo za Bibi Harusi za kuvaa siku ya Ndoa Pamoja n Harusi lakini wao hawakufanya hivyo ingawa walikuwa na Nguo ambazo tayari zilikuwa zimetumika.

Kwa upande wa Mchungaji aliyekuwa anataka kufingisha Ndoa hiyo ambaye pia ni Askofu wa Kanisa hilo, Mchungaji Kenan Mpalala alipoulizwa kuhusu hali hiyo amesema kwa mujibu wa taratibu za Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 8 pingamizi litolewe ndani ya siku 21.

Amesema upande wa Wazazi wa Mwanamke ulishindwa kuwasilisha pingamizi lao kanisani kabla ya Siku 21 badala yake walifika kutoa malalamiko kuhusu kutomaliziwa kwa mahali jambo ambalo alisema yeye kama Mwandikisha Ndoa halimhusu bali pande mbili wanatakiwa kulimaliza kabla ya Ndoa.

Naye Bwana Harusi Mtarajiwa Fadhili Mahenge(28) alipoulizwa kuhusiana na suala hilo huku akiwa tayari Kanisani kwa ajili ya Kufungishwa Ndoa alisema anachosubiri ni hatma ya Wazazi wa Mwanamke kama wanaweza kumwachia Mkewe iliwanachodai awe anamalizia taratibu.

Amesema yeye kama yeye kwa sasa hana fedha zozote za kuweza kumalizia anachodaiwa zaidi ya kuomba busara za wazazi wa Mwanamke kumruhusu Ndoa ifungwe ndipo aweze kulipa Mahari anayodaiwa kwa awamu kutokana na hali yake ya kiuchumi kuwa Mbaya.

Ameenda mbali zaidi kwa kusema kama Wazazi wa Mwanamke wataendelea kuwa na Msimamo huo basi hata yeye ataomba arudishiwe kile alichokitoa awali ili ajipange upya kwa ajili ya ndoa baada ya kukamilisha madai yao.



Hadi tunaingia mtamboni Mbeyayetu ambayo ilikuwepo sehemu ya tukio timu ya usuluhishi ilikuwa ikiendelea na kazi yake ikiongozwa na Mchungaji, Mwenyekiti wa Mtaa na Mzee Maarufu ambaye ni Katibu wa Chama cha Wakulima (TASO) kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Ramadhani Kiboko, huku muafaka ukiwa haujapatikana.

Na EZEKIEL KAMANGA,wa KAMANGANA MATUKIO BLOG