m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Monday, 15 April 2013

Dar yarejea enzi za ujima

Abiria wakigombea basi dogo katika kituo cha mabasi ya daladala Ubungo jijini Dar es Salaam jana.
Wakati nauli mpya za daladala, mabasi na treni zikianza kutumika rasmi leo, hali ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam imezidi kuwa mbaya kutokana na mabasi kuwa machache na hivyo kusababisha abiria kulazimika kusafiri kwa malori na magari mengi madogo huku wakitozwa nauli kubwa.
 
Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE umebaini kuwa maeneo ambayo yamekumbwa zaidi na tatizo la usafiri ni kutoka Mwenge kwenda Tegeta, Mwenge-Kibaoni, Ubungo-Mbezi, Ubungo-Mbagala, Gongolamboto-Mwenge na Ubungo kwenda Mlandizi.
 
Kutokana na ukosefu wa daladala kwenye maeneo hayo, kwa takribani wiki moja sasa wananchi wamekuwa wakitumia malori, Toyota Noah, Bajaj, Pick Up, teksi pamoja na Toyota Coaster ambazo hazijasajiliwa kuchukua abiria jijini hapa.
 
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa kutokana na ukosefu wa daladala, hali hiyo imetoa fursa kwa magari yaliyoanza kutoa huduma ya usafiri kwenye maeneo hayo kutoza abiria nauli kubwa ambayo haipo katika viwango vya nauli vilivyopangwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Usafiri wa Majini na Nchi kavu (Sumatra). Nauli inayotozwa na wamiliki magari hayo mfano kutoka Mwenge hadi Tegeta, Mwenge-Bunju, Mwenge-Kibaoni ni Sh.1,000 hadi 2,000 kwa mtu mmoja badala ya Sh. 300 au 400 ya sasa.
 
Kutoka Ubungo kwenda Mbezi, Ubungo-Mbagala, nauli zinazotozwa ni kati ya Sh. 500 hadi 1,000 badala ya Sh.300 wakati kutoka Ubungo-Mlandazi ni Sh.1,000 hadi 2,500.
Magari yaliyobainika kutoza nauli kubwa ni yale ambayo hayajasajiliwa na Sumatra kutoa huduma ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam na yaliyoiba njia.
 
Aidha, daladala ambazo zimesajiliwa kutoa huduma jijini hapa, zinaongoza kukatisha ruti (kuiba njia) na zinafanya hivyo ziweze kurejea mapema vituoni kuchukua abiria wengine hali ambayo inakuwa ni faida kwao. 
 
Mathalani, katika kituo cha Mwenge inapofika jioni, gari za ruti ya Tandika-Mwenge kupitia barabara ya Ali Hassan zimekuwa zikipakia Ubungo na kisha kushusha abiria wote na kupakia tena kwenda Bugurudi na zinapofika hapo hupakia kwenda Tandika.
 
Wakati mwingine, gari hizo zinapofika Ubungo hurudi tena Mwenge kupakia abiria.
 
Wakizunguma na NIPASHE kituo cha Ubungo, abiria waliokuwa wakisafiri kwenda Mbezi Luis, walisema tatizo la usafiri limekuwa sugu na kwamba wakati mwingine wanachukua zaidi ya saa tano kupata gari.
 
Amon Kisimbo mkazi wa Mbezi Luis alisema tatizo la usafiri katika jiji la Dar es Salaam linasababishwa na msongamano wa malori na kwamba serikali inatakiwa kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyowahi kutolewa mwaka 2009.
 
Kisimbo ambaye alidai alikuwa miongoni mwa watu walioshiriki kuandaa mapendekezo hayo katika tume iliyoundwa na serikali, alisema pendekezo walilotoa ni kutaka Bandari ya Dar es Salaam ihamishwe kutoka ilipo sababu inasababisha malori kupita katikati ya jiji na hivyo kusababisha msongano usiokuwa wa lazima. Ofisa Mfawidhi wa Sumatra, Kanda ya Mashariki, Conrad Shio, akizunguza na NIPASHE jana alisema kutokana na ukiukwaji wa sheria za barabara unaofanywa na wenye magari hayo, magari 74 yamekamatwa kutokana na makosa mbalimbali.
 
Shio alisema magari 36 yamekamatwa kwa kukatisha ruti, 18 kwa kuiba ruti na magari 20 yamekamatwa kwa kutoza nauli kubwa.
 
Alisema magari ambayo yamekamatwa kwa kosa la kukatisha ruti wamiliki wake watatakiwa kwenda Sumatra na mkataba wa madereva wengine na hao waliosababisha kosa hilo hawataruhusiwa kufaya kazi ya udereva mahali popote nchini.
 
Alisema tatizo la ukosefu wa magari katika baadhi ya maeneo linatokana na kwamba Sumatra imesimamisha usajili katika ruti ya barabara ya Ali Hasani Mwinyi-Kilwa kwa sababu kuanzia Julai mwaka huu wamiliki wa daladala watatakiwa kujiunga katika kampuni ili kutoa huduma ya usafiri kwenye ruti hiyo.
 
Alisema siyo kweli kwamba daladala zimeadimika na kwamba baadhi ya wamiliki wanakwepa kusajili magari yao kwenye njia zenye foleni kubwa kama Mbezi-Kimara hadi Kivukoni au Kariakoo.
 
MWAKYEMBE ABARIKI NAULI
Serikali imebariki ongezeko jipya la nauli za mabasi yanayotoa huduma mijini, ya masafa marefu na treni hivyo kuziruhusu kuanza kutumika rasmi leo.
 
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, aliwaambia wanahabari jana mjini Dodoma kuwa nauli mpya imeongeza Sh. 50 kwa mwanafunzi na Sh. 100 kwa watu wazima; hivyo daladala zitatoza Sh. 400 badala ya 300 na wanafunzi Sh. 200 badala ya Sh. 150.
 
Alisema  serikali imeridhia ongezeko la nauli lililotangazwa na Sumatra, baada ya kuhakiki na kujiridhisha kuwa ongezeko hilo lilizingatia mchakato wa kupandisha nauli na viwango viliridhiwa na wadau wanaowakilisha maslahi ya wanaotoa na wale wanaotumia huduma hiyo.
 
“Mimi kama Waziri wa Uchukuzi sina tatizo na ongezeko hili dogo la nauli za daladala tatizo langu ni tabia ya Watanzania kukacha vikao halali vinavyojadili mambo yanayotuhusu na kusubiri kuja kulalamika baadaye,” alisema Dk. Mwakyembe.
 
Alisema hayo akiwakosoa wananchi na asasi nyingine kulalamikia nauli nje ya utaratibu licha ya vikao vya kuwataka kutoa maoni kupitia Sumatra kutangazwa na kuwataka wananchi wajitokeze wakati maombi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri ya kupandisha nauli yalipokuwa yanajadiliwa.
 
Waziri Mwakyembe alisema maombi ya kuongezwa nauli hiyo mpya yalitolewa baada ya wadau wakiwamo Baraza la Taifa la Walaji wa Huduma zinazodhibitiwa na Sumatra, Chuo cha Usafirishaji, vikiwamo vyama vya watoa huduma vya madereva vya kutetea abiria na wanahabari, kuridhia.
 
“Kulikuwa na mvutano mkubwa wamiliki wakitaka nauli iongezeke na wawakilishi wa abiria wakitaka nauli ibakie ile ile iliyotangazwa mwaka 2011. Ndipo maamuzi  ya nyongeza ya nyongeza ndogo yakawa Sh. 100 na Sh. 50 kwa mwanafunzi yakaafikiwa,” alisema.
 
Aliongeza kuwa wawakilishi wa abiria na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji waliamriwa kuwa iwapo kuna upande usioridhia ukate rufaa kwenye Baraza la  Ushindani, lakini hakuna aliyefanya hivyo.
 
Wiki iliyopita Waziri Mwakyembe alisema wizara hiyo itapitia nauli hizo kutokana na malalamiko mengi kutolewa na wananchi wakipinga nyongeza hiyo.
Imeandikwa na Gaudensia Mngumi, Dodoma na Thobias Mwanakatwe, Dar
CHANZO: NIPASHE

Baadhi ya wadaiwa wa Bodi ya Mikopo wako taabani

http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/10881-baadhi-ya-wadaiwa-bodi-ya-mikopo-wako-taabani

Gesi ni hatari, Zimamoto wawahi kuokoa.



Gari la zimamoto likiwasili eneo la tukio
Leo asubuhi muda wa saa 3:30 kumetokea mlipuko mkubwa kwenye Glosary ya Kipingu eneo Mtaa wa Sae karibu kabisa na kituo cha Sae. Mlipuko huo wa moto umetokana na jiko la gesi lililokuwa likiwashwa ili kupasha supu na ndipo likalipuka na kuanza kuwaka moto mkali. Moto umezua balaa kubwa kwani kutokana na ukosefu wa vifaa vya tahadhari  vya zima moto na elimu ya majanga watu wakaanza kuzima kwa maji na mchaka lakini ikawa ni kama kuuchochea zaidi. Baada ya kushindika kuzima moto uliokuwa ukiwaka kwenye mtungu wa gesi na kuendelea kusambaa kwenye vyombo vingine ndipo kijana mmoja jasiri maarufu kama KP akajitosa na kuuburuzia nje mtungi uliokuwa ukiwaka moto mkali. Hapo ndipo akawa ameokoa nyumba hiyo yenye maduka manne isiwake moto.
Zimamoto wawahi kuokoa, kinyume na desturi ya zimamoto ya kuchelewa mara wanapoitwa kwenye majanga ya moto kwani waliwasiri mara moja baada ya kupigiwa simu. Zimamoto wamewapongeza wananchi kwa kuweza kuokoka jingo kuwaka moto kwa kuutoa nje mtungi unaowaka moto. Askari wa zimamoto wakauzima moto uliokuwa unaendelea kuwaka kwenye mtungi wa Gesi.
Wasisitiza kutoa taarifa mapema kila mara janga linapotokea kuwakumbusha wananchi kuw ana namba za simu ya kiganjani mbali ya ile ya mezani ili kutoa taaarifa kwa haraka zaidi. Ikumbukwe kuwa mara nyingi zima moto wamekuwa wakilalamikia baadhi ya watu wasio waaminifu wamekuwa waktoa taarifa za uongo kupitia simu ya bure ya 111.
Ushauri wa bure kwa wote wenye majiko ya gesi ni bora wakanunua kifaa cha kuzima moto (Fire Extinguisher) ili watumie kuzima moto mara moto unapolipuka.
Namba za kiganjani za Zimamoto jiji la Mbeya ni
0755 651923
Tazama Picha kutoka eneo la tukio
watu wakushuhudia uzimaji wa mtungi

mtungi umezima

Askari akizima mtungi uliolipuka

 Hata boda boda walikuwepo kujionea wenyewe




 Moto umezimwa tayari kwa safari.
Picha zote na KII

Kwisha! UFARANSA YAPITISHA MUSWADA NDOA ZA JINSIA MOJA, SWEDEN NAKO KIMBILIO LAO

Vuta nikuvute imetokea katika bunge la senate nchini Ufaransa, ambapo mwisho wa siku iliamuliwa kupitisha kwa muswada wa sheria ya kuruhusu ndoa za jinsia moja nchini humo, licha ya upinzani mkali kutoka kwa wabunge wenye msimamo mkali, ikiwamo viongozi wa dini.
Uamuzi huu ambao umepitishwa Ijumaa taehe 12 Aprili 2013 na Ufaransa , taifa lenye asili ya katoliki, umekuja baada ya muda mrefu wa majadiliano, kama ambavyo Rais François Hollande alivyoahidi kwenye uchaguzi mkuu mnamo Aprili mwaka 2012, sera ambayo ilimfanya avune kura nyingi za wafuasi wa ndoa hizo.
Waziri wa Haki, Bi Christian Taubira. © Gouvernement
Mtetezi mkubwa wa muswada huo, waziri wa haki nchini huko, Bi Christian Taubira, amesemema kuwa muswada huo unakuja kutokana na umuhimu wake, hasahasa kwa watoto wanaoishi na wazazi wa jinsia moja, ili wapate haki zao sawa na watoto wa wazazi wa kawaida. na kwa mujibu wa muswada huu, basi wenye ndoa za jinsia moja, watarushusiwa kuasili watoto kwa ajili ya kuwalea.
Tumefanya hivi kwa sababu kuna watoto hawali chakula cha afya, wanakula pipi kwa wingi, na kadha wa kadha, hao pia tunawalinda - wanahitaji hilo. Christian aliwaambia maseneta mara baada ya kupitisha muswada huo, ambao utapitiwa tena February 2014 kwa ajili ya marekebisho.
Kwa upande wake, seneta wa chama cha UMP, Jean-Pierre Raffarin, amesema kuwa bado wataendeleza mpambano kwa kuwa bunge bado lipo, na kilichopo ni kwamba watakuwa wakiongea na wananchi wataobadili mawazo ili kuhakikisha muswada huu unaondolewa na kurejea katika hali ya mwanzo, yaani mume na mke na si vinginevyo.
Mpaka sasa ufaransa imegawanyika kuhusiana na ndoa za jinsia moja, ambapo mnamo January mwaka huu, takriban watu 340,000 waliandamana kupinga ndoa za aina hii, wakisisitiza Baba na Mama kwa familia. Ambapo wiki mbili baadae, kundi la watu takriban 125,000 walijitokeza mtaani kuunga mkono ndoa za namna hiyo.
Nchi ambazo zimeridhia ndoa za jinsia moja mpaka hivi sasa. © CBC
Ulaya ni bara ambalo nchi zake kadhaa zimeruhusu ndoa za namna hii, ambapo kwa watu ambao nchi zao haziruhusu, wamekuwa wakikimbilia huko ili kuonana na kuishi kwa sheria za huko. mfano mmojawapo ni mashoga wawili Waganda, ambao walikimbia nchi yao na kuelekea Sweden ili kuonana kutokana na nchi yao kukataza vitendo vya ushoga na usagaji.
Wadau wa Gospel Kitaa walio nchini Sweden, walifanikiwa kupata tukio hilo kama lilivyofanyika mwezi wa kwanza kwa kamera, na hatimaye mdau Nahshon Kamugisha kuzirusha kwa GK.


Jimmy na Lawrence wakiwa na mashoga wenzao wakati wa sherehe ya 'kuonana'.
Gospelkitaa.com

Maajabu Geita:Aliyefariki miaka mitano iliyopita afufuka

mwanamke anayedaiwa kufariki miaka mitano iliyopita 


Posted  Jumapili,Aprili14  2013  saa 24:51 AM
Kwa ufupi
Inadaiwa kwamba Flora Onesmo (45) alifariki Februari 28, 2008 katika Hospitali ya Wilaya ya Geita na kuzikwa katika Kijiji cha Nakasenya, Kata ya Butundwe, lakini juzi alfajiri alikutwa ameketi nje ya nyumba ya dada yake aitwaye Monica James, anayeishi Kasamwa.Share

Geita: Mji wa Geita na maeneo ya jirani juzi ulikumbwa na taharuki ya aina yake, pale mwanamke ambaye anadaiwa kwamba alifariki miaka mitano iliyopita alipoonekana akiwa hai katika eneo la Kasamwa.
Inadaiwa kwamba Flora Onesmo (45) alifariki Februari 28, 2008 katika Hospitali ya Wilaya ya Geita na kuzikwa katika Kijiji cha Nakasenya, Kata ya Butundwe, lakini juzi alfajiri alikutwa ameketi nje ya nyumba ya dada yake aitwaye Monica James, anayeishi Kasamwa.
Aliyekuwa wa kwanza kumwona Flora ni mdogo wake aitwaye Monica Onesmo ambaye baada ya kuamka saa 11:00 alfajiri nyumbani kwa dada yake, alimwona mwanamke aliyekuwa ameketi nje ya nyumba hiyo, lakini alimfananisha mwanamama huyo na marehemu dada yake.
“Baada ya kumwona nilimwita mtoto wake tunayekaa naye na nikampigia simu dada (Monica) ambaye alikuwa amelala chumba kingine nikamwambia kwamba nimeamka na kumkuta mwanamke amekaa hapa nje, lakini kila nikimwangalia anafanana na marehemu dada yetu,”alisema Jubili na kuongeza kwamba alipowaita wote walitoka nje.
Alisema mtoto wa Flora (marehemu anayedaiwa kufufuka) anaitwa Rebeka Elisha (16) na kwamba walimchukua tangu 2008 wakati mama yake huyo alipofariki dunia katika Hospitali ya Geita ambako alikuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa ini.
Rebeka ambaye ni mtoto wa nne wa Flora alisema: “Mama mdogo alituita sisi tulikuwa tumelala akasema kwamba nje kuna mwanamke ambaye anafanana na marehemu mama yetu, ndipo na sisi tukatoka na kweli kumwangalia alikuwa ni yeye kabisa.”
Alisema walipomuhoji mama yake huyo kwamba ametokea wapi, aliwaeleza kuwa ametoka eneo la Katoro kwa mganga na aliletwa na watu ambao hakuwatambua Alhamisi saa 1:30 usiku ndani ya gari na watu hao walimshusha kwa mtu aitwaye Juma Luchunga ambaye ni jirani na dada zake hao.
Kauli ya Flora
Akizungumza na waandishi wa habari, Flora alisema yeye ni mkazi wa Katoro na kwamba alitokea Katoro nyumbani kwa mganga wa jadi ambaye hata hivyo hakumtaja kwa maelezo kwamba wataalamu wake (majini) wamemkataza.
“Nilikuwa naishi kwa mganga wa kienyeji ila alikuja mwanaume wakati nikiwa pale akaninywesha dawa kisha tukapakizwa kwenye gari na watu wawili ambao sikuwatambua, mmoja mwanamke na mwingine mwanaume mpaka hapa Kasamwa tukashushwa saa 1:00 jioni,”alisema Flora.
Alisema alipofika Kasamwa alikwenda kunywa uji kwa mama mmoja ambaye pia hakumtaja na kwamba baadaye alipelekwa nyumbani kwa mtu mwingine saa nne usiku, lakini watu wa nyumba hiyo walipomwona walimwambia: “Hapa si kwako twende tukupeleke kwa ndugu yako” na ndipo wakampeleka kwa dada yake ambako aliketi nje hadi alfajiri.
Flora alisema kabla ya kuishi kwa mganga alikuwa akiishi porini ambako alitupwa na watu asiowafahamu na baadaye aliokotwa na wasamaria wema ambao ndiyo walimpeleka kwa mganga ambako alikuwa akiishi muda wote.
Endeleahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1747968/-/129ypge/-/index.html

Sunday, 14 April 2013

Israel marks Memorial Day


Watch Video

Play Video
Israel is entering one of its most emotionally charged weeks of the year. On Sunday, the country held a Memorial Day ceremony for the Israeli Defense Forces’ Fallen Soldiers at Jerusalem’s Ammunition Hill.
Memorial Day will run from Sunday to Monday evening. It will be followed by the country’s 65th Independence Day celebration. Both holidays keep with Jewish tradition, in which sunset marks the beginning of a new day.
Israel’s Independence Day marks the end of the British Mandate. The country’s first prime minister, David Ben-Gurion, declared Israel’s independence in 1948.
CCTV

Venezuelans vote on future of "Chavista" socialism



CARACAS | Sun Apr 14, 2013 4:31pm EDT
(Reuters) - Venezuelans went to the polls on Sunday to vote whether to honor Hugo Chavez's dying wish for a longtime loyalist to continue his self-proclaimed socialist revolution or hand power to a young challenger vowing business-friendly changes.
Acting President Nicolas Maduro had a double-digit lead over opposition challenger Henrique Capriles in most polls heading into election day, buoyed by Chavez's public blessing before he died from cancer last month. But the gap narrowed in recent days, with one survey putting it at 7 percentage points.

http://www.reuters.com/article/2013/04/14/us-venezuela-election-idUSBRE93C0B120130414 

Saturday, 13 April 2013

Yes! President Uhuru meets Raila, Kalonzo


Uhuru and Ruto share a light moment with Odinga and Musyoka at State House Nairobi
By PPS
President Uhuru Kenyatta and his Deputy William Ruto Saturday at State House Nairobi met and held talks with CORD leaders Hon. Raila Odinga and Hon. Kalonzo Musyoka who paid him a courtesy call.
During the meeting, the CORD leaders conveyed their message of goodwill to the President and his deputy saying they wished them well in running the country.
In light of the recently concluded general election that was closely contested, the talks also touched on the need to bring Kenyans together and unite the country.
During the meeting, President Kenyatta expressed the willingness of the Jubilee leadership to nurture a working relationship with all Kenyans irrespective of their political affiliations in order to strengthen national unity.
The leaders called upon Kenyans to now rise above the differences that arose during the electoral period and join hands in nation building as members of the same Kenyan family.
Source; kcb.co.ke

Friday, 12 April 2013

We offer best services, read

KII offered services are available for you, Karibu sana

MAAJABU, MAKANISA NDANI YA MAPANGO

Mapango yana mchango mkubwa katika historia ya Uyahudi na Ukristo kwa ujumla. Daudi alijificha kwenye pango wakati akimtoroka mfalme Sauli, nyaraka muhimu za 'bahari ya shamu'pia zilipatikana kwenye pango, na wakristo pia wamekuwa wakikutana kwenye mapango kwa ajili ya kuabudu.
Huko Bulgaria, katika mji wa Mihalich - kuna pango ambalo kanisa lilikuwa likikutana. Wanahistoria na wataalamu wa mambo ya kale wanaamini kuwa kanisa hilo la pango limetumika mnamo karne ya 10.

 Flickr/Klearchos Kapoutsis - Creative Commons
Kwa mujibu wa tovuti ya a view on cities, Kanisa la pango la Mtakatifu Stefano mjini Budapest, Romania, lilifungwa na wakomunisti mwaka 1951, na kisha kufunguliwa tena mwaka 1989. Kanisa hilo lilikamilishwa ujenzi wake mwaka 1931.
© Flickr/Robot B - Creative Commons
Pengine kanisa la pango ambalo linafahamika sana duniani ni lile la Misri, ambapo wa'Zabbaleen', watu wanaokusanya taka jijini Cairo wanaabudu.
Kwa mujibu wa mtandao wa wikipedia, kuna makanisa ya pango saba yaliyojificha kwenye mapango ya mlima Mokattam. Kanisa la Mtakatifu Simon the Tanner ndilo kanisa kubwa mashariki ya kati, likiwa na uwezo wa kuchukua watu waliokaa 20,000.

© Flickr/Roaring Jellyfish - Creative Commons



Kanisa hilo limechuka jina la Mtakatifu Simon the Tanner ili kumuenzi, mkristo wa dini ya Coptic kutoka karne ya kumi.
Urithi ambao umeachwa na makanisa ya handaki ni mkubwa na wa kipekee.
Mtume Paulo anaandika kwenye waraka wa Waebrania sura ya 11 kuhusu waamini waaminifu ambao wameonesha imani ya kipekee.
"(Watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi" Waebrania 11:38
Mpaka hivi sasa, kuna wakristo ambao huabudu kwenye makanisa yaliyo kwenye mapango.

Thursday, 11 April 2013

G8 wailaani Korea Kaskazini

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa manane yaliyoendelea zaidi kiviwanda wameungana kuilaani Korea Kaskazini, na kuitaka nchi hiyo kukomesha mara moja kutoa vitisho vya kivita
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Wester Welle, amesema katika siku ya pili ya mkutano wa mawaziri hao unaoendelea jijini London, Uingereza, kuwa mataifa yote ya G8 yanaaminini kuwa kuongezeka kwa matamshi hayo ya kuchochea vita kutoka kwa Korea Kaskazini lazima kusitishwe.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle
"Suala la kwa nini matamshi hayo ya kuchochea vita yanaongezeka – ingawa ni muhimu, lakini halina uzito mkubwa. Muhimu zaidi ni kwamba matamshi hayo hayapelekei kuripuka kwa vita. Na ndio maana ni muhimu sasa kuona jumuiya ya kimataifa ikiwajibika na kuzungumza kwa sauti moja. Siyo pekee nchi za magharibi zinazobidi kuwa na msimamo mmoja, bali pia China na Urusi. Maoni yangu ni kwamba nchi hizi mbili pia zingependelea hivyo," alisema Wester Welle.
Korea kaskazini imetoa vitisho dhidi ya Korea Kusini, Japan na Marekani na inaonekana kujiandaa kufanya majaribio kadhaa ya makombora ambayo wadadisi wanasema huenda ikayafanya kwa wakati mmoja. Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza, William Hague, alisema nchi iko njia panda hivi sasa, na inaweza kuishia kuwa taifa lililosambaratika na kutengwa, iwapo itashindwa kushiriki mazungumzo.
Tisho la mfululizo wa majabirio ya makombora
Jeshi la Korea Kusini limenukuliwa leo likisema kuwa Korea Kaskazini inaweza kufanya majaribio hayo ya makombora muda wowote, na kwamba mitambo ya kuvurumishia makombora hayo imekwishawekwa katika pwani ya mashariki ya nchi hiyo. Shirika la habari la Yonhap la mjini Seoul limesema kuwa mitambo karibu mitano imeonekana katika mkoa wa mashariki wa Hamkyung Kusini.
Shirika hilo likimnukuu afisa wa serikali ya Korea Kusini ambaye halikumtaja jina, limesema kuwa zipo dalili za wazi kuwa Korea Kaskazini inaweza kuvurumisha makombora aina ya Musudan, Scud na Nodong kwa wakati mmoja. Makombora ya Scud yana uwezo wa kwenda umbali wa kilomita kati ya 300 na 500, na Nodong yanaweza kwenda kati ya kilomita 1,300 hadi 1,500.
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa yaliyoendelea zaidi kiviwanda G8 wakiwa katika mkutano wao mjini Londo Uingeraza Alhamisi 11.04.2013. Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa yaliyoendelea zaidi kiviwanda G8 wakiwa katika mkutano wao mjini Londo Uingeraza Alhamisi 11.04.2013.
Wakati wasiwasi ukizidi kutanda katika rasi ya Korea, katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami NATO, Anders Fogh Rasmussen, amewasili Korea Kusini kwa ajili ya mazungumzo, katika ziara ya kwanza kabisa ya kiongozi huyo wa jumuiya hiyo ya kijeshi.
Korea Kusini pia imeisihi Korea Kaskazini kufungua tena eneo la viwanda la Kaesong lililofungwa tangu siku ya Jumanne. Eneo hilo linaendeshwa kwa pamoja kati ya Korea mbili, na waziri wa muungano wa Kusini, Ryoo Kihl, ameitaka kaskzini irudi katika meza ya mazungumzo. Lakini afisa kutoka wizara hiyo alisema baadaye kuwa taarifa hiyo ya waziri Kihl Jae haikuwa pendekezo rasmi la kuanzisha tena mazungumzo.
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/dpae,
Mhariri: Jospehat Charo

DW

Wednesday, 10 April 2013

Uhuru aapishwa, ICC kunani?

Kenya's President elect Uhuru Kenyatta waves to guests as he arrives for his official swearing-in ceremony at Kasarani Stadium in the capital Nairobi, April 9, 2013. REUTERS-Thomas Mukoya (KENYA - Tags: SOCIETY POLITICS ELECTIONS PROFILE)Hatimaye Uhuru Kenyata ameapishwa leo kuwa raisi wa nne wa Kenya. Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa rais huyu kijana lakini kubwa na la kihistoria ni ule msukumo wake wa kugombea urais japo ana kesi katika mahakama ya ICC. Si jambo rahisi na binafsi naweza kumuona kuwa ni mtu jasiri na mfuasi wa UKWELI yaani alitaka aone wakenya wakiamua kumkubali au kumkataa na si wale vibaraka waitwao ICC. Uhuru anaungana na Obama kuwa vijana walithubutu kufanya kitu kisichowezekana na KIMEWEZEKANA. Wote Uhuru na Ruto wameudhihirishia ulimwengu uongo na uchonganishi wa ICC kwamba wakati yenyewe inawaona ni wahalifu nyumbani wameonekana mashujaa na watu wanaohitajika kuwaongoza.
Binafsi nimekuwa na wasiwasi mkubwa juu ya the Hegue ikiwa kweli ni mahakama ya kweli na ya usawa kwa watu wote, nahisi ipo kwa ajili ya waafrika na zaidi kuwachonganisha ili kuendeleza ukoloni mamboleo. Inawezekanaje Uhuru na Ruto wakutwe na kesi lakini Odinga aliyeamuru watu na zaidi vijana waingie mtaani kupinga matokeo? si mtaani ndiko ukageuka uwanja wa mapigano?
Aaah nashikwa na kigugumizi na hivyo acha nimalizie habari kuapishwa, jambo lililonigusa kwa Uhuru ni ule msimamo na kujiamini na zaidi kusimama yeye kama yeye, ndio marais waliokosekana Afrika watu wanaoweza kuonyesha msimamo na kutoa maamuzi mazito ya kuleta mageuzi katika nchi zao. Afrika sasa inahitaji viongozi ambao hawatakuwa tayari kutishwa na vijibwa vya kizungu ambavyo kwa ajili ya kudoea maliasili zetu vinaleta uchonganishi kila kukicha. Binafsi sipingi kushtakia kwa viongozi waahalifu bali nataka nione wakishtakiwa Afrika, nataka kuona ICC ya kiafrika kama ile ya Arusha ya Mauaji ya kimbari. Mbona Mahakama ya Arusha hatujasikia ikishutumiwa na imefanya kazi zake kwa amani pasipo mgogoro wowote? Waafrika tuhukumiane wenyewe hata sisi tuna roho kama za wazungu rangi siwape shida. Sasa nafikiri ICC itabidi wafikiri upya. Uhuru kaapishwa ICC kunani? lazima wapate kigugumizi
Pia sitakuwa nimetenda vyema kwa kutomgusa Odinga yule rafiki yangu wa mwaka 2007, nasema rafiki yangu maana nilimpigia chapu katika uchaguzi ule hasa katika hadithi zetu vijiweni. Lakini Odinga huyu ambaye kwa kushindwa kwake watu elfu walikufa baadaye akapewa cheo kipya cha Waziri Mkuu badala ya kutekeleza ahadi akashughulika na cheo chake tu, na hapo akajipandishia mshahara wananchi wakibaki kuhaha tu na umaskini. Leo Odinga pasipo aibu anarudia kusema ameibiwa kura, mimi si mkenya lakini naelewa fikra za wakenya hasa linapokuja suala la utawala na ukabila. odinga kachakachuliwa kula na kutotimiza Ahadi kwake na roho ya ukabila iliyotawala kenya nas si vinginevyo. Jambo la ajabu kabisa ni vile Odinga asivyokomaa kisiasa kwa kuamua kukimbilia Afrika Kusini wakati mwenzake akiapishwa, hakika kaonyesha kutokuwa Mzalendo na zaidi kuwa kwake muhimu ni cheo na si utumishi.
Nampa Hongera Uhuru na Ruto na zaidi wapate changamoto ya kuwathibitishia wakenya na ulimwengu kuwa wanaweza kuleta maguzi kinyume na matariajio ya The Hegue.