m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Wednesday, 22 January 2014

ZZK NA WARAKA WA MAREHEMU CHACHA WANGWE KWA CHADEMA

Ndugu zangu watanzania
Naomba kwanza nikiri kwamba mimi si mwanachama wala shabiki wa chama chochote nchini, niliwahishabikia CCJ kabla hakijauawa katika uchanga wake. Nazungumzia uanachama na ushabiki na tena ushabiki unagawanyika zaidi kwa mtazamo wangu upo ushabiki wa dhati na ule uchwara. Shabiki yupo tayari kutetea timu au chama chake pasipo kujali ukweli wenyewe, shabiki huitaji kushinda kwa maneno, hupenda kuongoza kijiwe na kamwe hakubali kuumizwa moyo wake kwa ushindi wa mpinzani wake. Kama ni mfuatiliaji wa machapisho ya blogu hii utabaini kuwa nimeguswa sana na mnyukano wa kisiasa ulioanza mwishoni mwa mwaka hadi sasa kwenye chama kikiuu cha upinzani nchini. Yalipotokea ya Zitto Zuberi Kabwe maarufu kama ZZK na mkakati wao na Komredi Mwigamba na Dkt Kitila Mkumbo ghafla nikakumbuka yaliyompata Chacha Wangwe. Nilipokumbuka hayo ndipo nikadhamiria kuusaka waraka wa Marehemu Chacha Wangwe ili kujiridhisha ikiwa mawazo yangu ni halisi. Nimebaini mambo kadhaa
1. katika siasa za nchi hii kuhoji ni dhambi iwe kwa upinzani au utawala kwani ndio matokea ya akina Chacha wangwe, Shibuda alipohoji CCM, Dkt Ulimboka na sakata la madaktari na Sasa ZZK na makomredi zake
2. Hoja hutendewa kazi kutokana na nafasi ya anayehoji... si suala la uzito wa hoja.
3. Katika meza ya wapinzani anayehoji ni wa CCM na katika kiti cha CCM anayehoji ni mpinzani.
Mwisho kabla ya kuchapisha waraka huo niseme kwamba nimeuchapisha ili kuwapa nafasi watanzania uwanja wa kufikiri wenye mapana na marefu kwani naipenda nchi yangu na ni ndoto zangu siku moja kuwa na nchi yenye siasa safi. Pia lazima tukubali uzito wa hoja na si uzito wa anayehoji, ikiwa hoja ni nzito itendewe kazi na si kutuhumu aliyehoji.
Nagona

WARAKA WA MAREHEMU CHACHA WANGWE KWA CHADEMA
Jumamosi, June 28 mwaka huu wajumbe kadhaa wa Kamati Kuu ya CHADEMA walidai kuwa wamesitisha Umakau Mwenyekiti wangu katika kikao kilichofanyika mjini Dodoma siku hiyo. Kesho yake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. FREEMAN MBOWE akaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutaja sababu za kunisimamisha uongozi.

Inatosha tu kusema kuwa sababu zote alizotoa ni za uzushi kama ile inayodai kuwa mimi navujisha siri za chama kwa viongozi wa CCM bila hata kutaja siri hizo, au kusema nimezitoa lini, wapi, na kwa kiongozi yupi?Kikao hicho kinachosemekana kunisimamisha uongozi, kilikuwa na wajumbe 31 ambao takribani nusu hawakuwa na uhalali wa kupiga kura kinyume cha katiba na kanuni za CHADEMA kwa vile walikuwa wameandaliwa kwa kazi hiyo. Wajumbe 7 walikataa kushiriki njama hizo.

Kufuatia jaribio hilo la kunivua uongozi kutokubalika kwa wanachama walio wengi wa CHADEMA , Mwenyekiti MBOWE na wafuasi wake wameendelea kuhaha kwa kuongeza sababu nyingine mbalimbali ili kuhalalisha njama zao. Sasa hivi wameingia hatua ya kuwashawishi wanachama wa Tarime eti wanifukuze uanachama.Kwa kuzingatia katiba, kanuni na taratibu za CHADEMA, nilichokifanya mimi baada ya kubaini njama zao ni kukata rufaa kwa Baraza Kuu la Chama, kupinga upotoshaji unaofanywa chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE anayeonekana kutaka kuendesha chama kinyume na matarajio ya wanachama walio wengi.Hivyo basi zipo habari za uhakika kuwa kikao hicho cha Baraza Kuu hakitaitishwa ama kabisa, au kitacheleweshwa kwa makusudi, kwa visingizio mbalimbali ikiwemo kutokuwa na fedha za kukidhi gharama za kikao hicho.

Naomba nikiri kuwa ninakerwa sana na mtiririko mzima wa sakata hili linalozua mgogoro unaokiyumbisha chama. Ukweli ni kwamba mimi niligombea Umakamu Mwenyekiti nikiwa na agenda ya kufufua uhai wa chama kwa kukaripia vitendo visivyostahili katika kuendesha chama. Agenda yangu haijabadilika. Yote niliyoyasema wakati nagombea nafasi hii yanafahamika kwa wana CHADEMA wote.

Walikuwepo walioyalalamikia na walikuwepo walioyapongeza matamshi yangu hayo.Mwisho wa yote wana CHADEMA waliridhika kuwa ajenda yangu ilikuwa sahihi na hivyo wakanichagua kuwa Makamu Mwenyekiti. Hivyo basi hata kama ni kweli kuwa ulikuwepo mvutano wakati wa kampeni ile, lakini hilo ni jambo la kawaida katika uchaguzi. Nijuavyo mimi hayo yalitakiwa yawe si ndwele nasi tugange yajayo kwani wanachama walikwisha fanya uamuzi halali kupitia kura zao.

Baada ya kuingia kwenye wadhifa wa Makamu Mwenyekiti Taifa, nilifanikiwa kuzungumza na Mhe. MBOWE kuhusu mambo, hususan yale, niliyoyapigania wakati wa kinyang?anyiro kile na kumuomba tukae chini na kutafuta jinsi ya kufanikisha azma hiyo.Ni imani yangu kuwa waraka huu utawasaidia wanaCHADEMA wenzangu na watanzania wote kwa ujumla, kuelewa vizuri ukweli wa mambo niliyoyapigania kabla ya kuwa Makamu Mwenyekiti, na ninayoendelea kuyasimamia hivi sasa nikiwa Makamu Mwenyekiti, na inshallah nitakayoyatekeleza baadae kama Taifa Mwenyekiti wa CHADEMA.

Kimsingi mambo tunayotofautiana na Mhe. MBOWE ni haya yafuatayo:-

MATUMIZI YA RUZUKU
CHADEMA hupata ruzuku ya Tshs. 66,000,000 kwa mwezi (Milioni sitini na sita). Mimi nasema si haba hasa tukizingatia chama kilikotoka. Naamini kuwa kiasi hiki cha fedha kikisimamiwa vizuri kinaweza kukirahisishia chama kujieneza katika ngazi zote toka Tawi, Wilaya, Mkoa na Taifa.

Si kweli kwamba matatizo yote yatamalizwa na fedha hizi lakini basi hata ofisi za chama zinaweza kuwa hai nchi nzima kitu ambacho kwa sasa hakipo. Mahesabu yanaonesha kuwa mtaji wa laki moja (Tshs.100,000/=) kwa wilaya moja nchini inatosha, hivyo kwa Wilaya 126 kwa mwezi jumla yake ni Tshs. milioni 12 (Tshs. 12,600,000/= ) zinahitajika ( Wilaya 126 x 100,000 kila wilaya = 12,000,000/=)Hata tukisema tupeleke kiasi hicho kwa kila jimbo la uchaguzi jumla yake ni Tshs. Milioni 23 (Tshs. 23,000,000/=) kwa maana ya majimbo 213 x 100,000 = 23,000,000/=.
Mhe. MBOWE anasema hizo ni pesa nyingi sana kwa uimarishaji wa chama. Mimi nasema hapana, kiwango hiki kwa kila Wilaya au Jimbo la uchaguzi ni muafaka kwani haba na haba hujaza kibaba.Chini ya uongozi wa Mhe. MBOWE na wafuasi wake hawastaajabu kuwa kati ya Tshs. 374,144,000.40 zilizopatikana kama ruzuku katika ya Januari 1 na Juni, 30, 2008, Tshs. 350,000,000/= zilitumika Makao Makuu ya CHADEMA na Tshs. 25,000,000/= tu ndizo zilikwenda Wilayani kuimarisha chama.Mimi naona mgao huu unayatukuza Makao Makuu ya
CHADEMA isivyostahili wakati huo huo ukidhalilisha chama nchi nzima.

MADENI YA UCHAGUZI
Kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mhe. MBOWE alitufahamisha wanachama kuwa alikuwa anakidai chama US $ 181,949.00 sawa na Tshs. 218,338,546. Mpaka sasa chama kimekwisha mlipa Tshs. 175,000,000/=Baada ya kupata wadhifa wa Makamu Mwenyekiti, na kwa kuzingatia takwimu zionekanazo hapo juu katika kulinganisha matumizi ya fedha Wilayani na Makao Makuu niliamua kumshauri MBOWE asitishe kujilipa deni kutokana na fedha za ruzuku kwani siamini kuwa kulipa madeni yaliyopita kunaendana na utaratibu wa usimamizi wa fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa toka serikalini.

Mhe. MBOWE alichachamaa na ndipo nilipomshauri kuwa kama ni hivyo basi atuthibishie pesa hizo anazodai alikikopesha chama ziliingia kwenye akaunti gani ya CHADEMA, kupitia hundi ipi, na lini? Nilimuomba pia kutaja ni kikao gani cha chama kiliidhinisha matumizi ya fedha hizo kwani kama hakuna ushahidi wa maidhinisho, ni dhahiri kuwa matumizi hayo hayakudhibitiwa na chama na kwa mantiki hiyo kuyafanya kuwa matumizi binafsi ya Mhe. MBOWE.Vilevile, nilimueleza kuwa matumizi ya fedha hizo alizodai alikikopesha chama yalikuwa yakinuka harufu ya UFISADI.

Stakabadhi zote kuhusiana na matumizi hayo zilionesha kuwa gharama za aidha ununuzi na / au ukodishaji wa vifaa hivyo, hazikutofautiana na viwango wanavyolipishwa watalii kwa huduma kama hizo, kwa maana ya gharama ya juu sana.Na kwa kuwa hata baada ya kuwa Mhe. MBOWE amekwisha lipwa zaidi ya nusu ya deni alilodai kuikopehsa CHADEMA, vifaa vyote yakiwemo magari, vipaza sauti na kadhalika vimebakia kuwa mali yake binafsi, basi bila kumficha nilimueleza kuwa huko ni kukinyonya chama kwa kukigeuza kitega uchumi cha watu binafsi.Kuhusu suala la kulipa madeni kupitia ruzuku ya serikali, nilimuomba Mhe. MBOWE afuatilie kwa Msajili wa Vyama vya siasa ili tupate ufafanuzi kama kweli fedha za ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa, inaweza kutumika kulipia madeni ya viongozi wa vyama hivyo yatokanayo na uchaguzi ili CHADEMA isiathirike kisheria.

Niseme kweli hapa kwamba, kwa vile wanaCHADEMA wengi walinichagua kuwa Makamu Mwenyekiti, na hata mimi mwenyewe tulikuwa wagombea wa nafasi za ubunge, udiwani n.k katika uchaguzi wa mwaka 2005 ningefarijika sana iwapo na sisi tungerejeshewa angalau chochote cha kufidia gharama zetu, kwa maana kwamba kama chama kimeamua kurudisha gharama hizo kiwalipe wote badala ya kulipa madeni kwa wateule wachache.

UTEUZI WA WABUNGE WA VITI MAALUM
Naamini ukweli wa suala hili hauna mjadala. Kwamba Mhe. MBOWE na wafuasi wake walighushi orodha ya majina ya viti Maalum badala ya kupeleka yaliyopendekezwa na Kamati Kuu sio siri.

Naamini hata Mhe. MBOWE anakubaliana nami kuwa suala hili si moja ya siri anazodai nimevujisha! Yamesemwa mengi juu ya mtafaruku uliojitokeza kuhusu viti maalum hadi baadhi ya waasisi wa chama wakataka kujitoa na hivyo kumlazimisha Mwenyekiti Taifa ( FREEMN MBOWE) na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kukiomba radhi kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kwa kukiuka katiba, kanuni na maadili ya chama katika suala hili la kugushi viti maalum.

Ni ukweli ulio wazi kuwa kitendo hicho cha upendeleo bado kina iumiza taswira ya CHADEMA. Chama kinaonekana kuendekeza ujanja ujanja kiasi kwamba watu na binti zao, wakwe zao, shemeji zao, waume wenzao, wachumba wa shemeji zao, wake wenza na kwa kiwango kikubwa watu wa kabila moja ndiyo wamekuwa sura ya CHADEMA bungeni.Katika hili nilichoweza kumueleza Mhe. MBOWE ni kuwa chaguzi mbalimbali tangu za Mitaa, Ubunge na Urais zinakaribia ni vizuri tufanye bidii kusambaza nguvu zetu nchi nzima tuwe na mtaji wa kura maeneo mengi ili kashfa kama hii isijirudie. Hii ni kwa msingi kuwa chama kikijitanua kutakuwa hakuna sababu ya kuwaona watu wa eneo fulani tu kuwa ndiyo mhimili wa CHADEMA na hivyo zikitokea fursa itakuwa rahisi chama kuwakilishwa na mtandao wake mpana badala ya koo au kabila fulani.Sasa kwa kuwa kuimarisha chama kitaifa maana yake ni matumizi ya fedha, nalo hili likawa nongwa ingawa kwa mtazamo wa Makao Makuu kulipa madeni kwa wateule wachache si nongwa.

Cha ajabu ni kwamba Mhe. MBOWE hakukana kuwa hili la viti maalum na hata upangaji wa ajira kwa ukabila una leta athari mbaya kwa mustakabali wa CHADEMA

Katika maongezi yangu nae nilikuwa wazi nilipotahadharisha kuwa:

1. Watanzania wakiendelea kuona kwamba CHADEMA inaendeshwa kwa misingi ya kikabila hawatajiunga na chama chetu na tutakosa wafuasi.

2. Watanzania wakiona kuwa sisi tumeweka mbele ukabila kuliko utaifa hawatatupa madaraka na kutawala kwa kuhofia yale yanayotokea nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Kenya na kadhalika ambako nafasi za raia wote zimehodhiwa na kabila moja na hatma yake watu wamechinjana kama kuku kwa kupinga hilo.
Pia nilimwambia kwamba, kwa jinsi sura ya uteuzi wa Wakurugenzi na watendaji wengine wa Makao Makuu inavyoonekana, sasa tayari chama chetu kimebatizwa jina la CHAMA CHA WACHAGA, na hii si kuwatendea haki raia wengine na makabila yao ambao wataonekana kama punguani kujihusisha na chama na ukabila.Yote haya ninayosema kuhusu ukabila, upendeleo na kadhalika sio dhana tu. Kufuatia malalamiko mengi yaliyokuwa yakisikika nchi nzima kuhusu masuala haya, Kamati Kuu ya CHADEMA ilikwisha unda Tume kutafuta ukweli wa mambo hayo. Tume hiyo ya watu watano iliongozwa na Mhe. Merky Lugendo Mziray ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA nayo imekwisha toa taarifa yake kwamba Makao Makuu ya CHADEMA yanatawaliwa na ubaguzi wa kikabila, kidini na kielimu.

UTENDAJI WA KIBABE
CHADEMA ni chama kilicho njia panda kwa sasa kutokana na utendaji wa kibabe wa Mhe. MBOWE. Ninafahamu jinsi vyama vingine vya upinzani hapa nchini kama vile NCCR ? Mageuzi vilivyoporomoka haraka haraka mithili ya nyumba ya mabua. Chama NCCR ? Mageuzi kilifikia mahali pazuri tu hadi watu wakaanza kufikiria kuwa kingekuwa chama mbadala kwa CCM.

kwa bahati mbaya uchu wa madaraka, ulafi wa ruzuku, na tabia za kimangimeza kwa pamoja vikakiathiri hadi kupoteza umaarufu wake.Na hata vyama vingine vya upinzani vina dalili hizo hizo japo kwa viwango vinavyotofautiana. Ila badala ya kujichunguza na kujua kasoro zetu, kila siku vyama vyetu, vimekuwa vikidai kuwa ni chama tawala ndicho kinachoviroga, kama ambavyo Mhe. MBOWE ameanza kuweweseka kupitia vyombo vya habari.Napenda kuthibitisha kuwa katika mgogoro unaopaliliwa sasa na Mhe. MBOWE ndani ya CHADEMA kutokana na ufisadi, ufuska, ulevi wa madaraka na umangimeza chanzo chake ni tabia yake ya kuendesha chama kibabe. Mathalan kumzuia Martin Mung?ong?o Mkurugenzi aliyechaguliwa kwa kura kutofanya kazi zake ndani ya chama, madai ya kupigana na watendaji wa chama ndani ya baa na vitendo vingine vya aina hiyo ni ushahidi tosha wa hulka hii.

Hadi sasa Mhe. MBOWE amefanikiwa kukizuia chama hiki kisifanye kazi ya siasa mkoa wa Dar es salaam kwa miaka minne.Ninavyoongea hivi sasa CHADEMA imekuwa ikikimbia vikao vya Democratic Union of Afrika (DUA), Muungano wa Vyama Vya Upinzani, uliofanikisha CHADEMA kujuana na Conservative Party ya Uingereza na Republican ya Marekani. Vyama dada hivi vyote vinaulalamikia uongozi wa CHADEMA kwa kufuja fedha ya misaada na kuwasilisha kwao risiti za kugushi, kama ilivyofanyiwa Conservative Party baada ya kutoa msaada wa Tshs. 78,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa baiskeli na pikipiki ambazo hazikununuliwa.Katika mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA huko Dodoma hivi majuzi tu, Mhe. MBOWE kwa kauli yake aliwatisha wajumbe kuwa alikuwa amethibiti uwezekano wowote wa wajumbe kujisikia huru kwa kutoa mawazo ambayo yangepingana na ajenda yake aliyoitoa ghafla kikaoni kunisimamisha Umakamu Mwenyekiti.

Mhe. MBOWE Alikifahamisha kikao kuwa alitoa taarifa kwa IGP, SAID MWEMA kuwa kuna wahuni ambao walitaka kuuchafua mkutano wake, naye IGP akahakikisha kuwa mkutano ule unalindwa kwa kiwango cha kushtua kama ambavyo hata vyombo vya habari vimethibitisha.Hayo ni baadhi tu ya mambo yanayobainisha Mhe. MBOWE ni kiongozi wa aina gani.

HITIMISHO
Kama nilivyokwisha sema hapo awali, sijaacha na sintoacha ajenda yangu ya kufufua uhai wa CHADEMA kwani ndiyo ahadi iliyofanikisha kuchaguliwa kwangu kuwa Makamu Mwenyekiti Taifa. Nilipopata wadhifa huo nilianza kuitekeleza ajenda hiyo kupitia mahojiano na Mwenyekiti MBOWE kuhusu matumizi ya ruzuku, madeni ya uchaguzi, uteuzi wa wabunge wa viti maalum, nafasi za ajira Makao Makuu, na kuhusu mwenendo wa chama Mkoa wa Dar es salaam.

Nilijikuta katika mvutano mkubwa kila nilipogusa eneo lolote katika haya. Nakiri kuwa kwa kiwango kikubwa sikuwa na uwezo wa kubadili mambo hayo yaliyokuwa yakiratibiwa kwa ukaribu na Mhe. MBOWE na wafuasi wake kwani sikupewa ushirikiano wa aina yoyote na chama pale Makao Makuu.

Ni vigumu kuamini, lakini ni kweli kuwa sikuwa na ofisi Makao Makuu, sikupewa vitendea kazi kama magari, vipaza sauti na/au vyombo vya habari, na sikuwahi kupata taarifa yoyote ya kiutendaji toka Makao Makuu.Kwa kuzingatia yote hayo, naomba nichukue fursa hii kuwashukuru kwa dhati wanachama wa CHADEMA mkoa wa Dar es salaam ambao kwa pamoja tulisimama kidete kufufua uhai wa chama hapa jijini. Niseme tu ushirikiano wao wa hali na mali uliniwezesha kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa na kimataifa.

Rai yangu kwa wana CHADEMA na wale wote wanaokitakia mema chama chetu na nchi yetu kwa ujumla ni kwamba kazi ya kupigania demokrasia ya kweli ndani na nje ya chama, kukiepusha chama na vitendo vya ukabila, migogoro, ubadhirifu, umangimeza, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote bado inaendelea na nawaombeni mniunge mkono kwa hali na mali katika vita hii.
UTANGULIZI.
Naamini tutashinda.
Mungu Ibariki CHADEMA
Mungu Ibariki TANZANIA
Mungu Ibariki AFRIKA
Chanzo:
 


Tuesday, 21 January 2014

Computer Basic Skills-Handout Coming Soon

Dear customer and supporter of KII be prepared to get Computer handout which will save students and the society from Computer Ignorance and join the computer expert family. 
Handout will be available for best price compared to contents.

 

Sunday, 19 January 2014

Serikali yawabeba waliofeli kidato cha pili


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa. Picha na Maktaba 
Na Fidelis Butahe, Mwananchi

Posted  Jumapili,Januari19  2014  saa 2:0 AM
Kwa ufupi
  • Licha ya matokeo hayo kutotangazwa hadi sasa, imebainika kuwa waliofaulu mtihani huo uliofanywa Oktoba 7 hadi 21 mwaka jana ni asilimia 62 tu, asilimia 31 wakitakiwa kukariri (kurudia) kidato cha pili mwaka huu, huku asilimia saba wakishindwa mtihani huo kwa mara ya pili.
Dar es Salaam. Wakati Watanzania wakisubiri matokeo ya kidato cha pili mwaka 2013, imebaini kuwa Serikali imetoa agizo kwamba wanafunzi wote waliofeli mtihani huo kuendelea na masomo ya kidato cha tatu, huku wakisoma mafunzo ya kurudia mtihani wa kidato cha pili.
Licha ya matokeo hayo kutotangazwa hadi sasa, imebainika kuwa waliofaulu mtihani huo uliofanywa Oktoba 7 hadi 21 mwaka jana ni asilimia 62 tu, asilimia 31 wakitakiwa kukariri (kurudia) kidato cha pili mwaka huu, huku asilimia saba wakishindwa mtihani huo kwa mara ya pili.
Jumla ya wanafunzi 531,457 walitajwa na Wizara ya Elimu mwaka jana kuwa watafanya mtihani huo.
Uamuzi huo wa Serikali ni tofauti na ule uliotolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa Novemba 4, mwaka 2012, kwamba kuanzia wakati huo mtihani wa kidato cha pili utakuwa ni wa mchujo na kwamba atakayefeli atatimuliwa.
Dk Kawambwa alisema matokeo ya mtihani wa kidato cha pili yatatumika kama kigezo cha kuchuja na kukariri kidato cha pili kwa watahiniwa watakaoshindwa kufikia wastani wa ufaulu wa alama 30.
Alisema mtahiniwa ataruhusiwa kukariri kidato cha pili mara moja tu na endapo mtahiniwa atashindwa mtihani kwa mara ya pili kwa mwaka utakaofuatia, itabidi aendelee na elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi.
Gazeti hili limeiona barua iliyoandikwa Januari 16 mwaka huu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kusainiwa na Katibu Mkuu wake, Profesa Sifuni Mchome, kwenda kwa wadau wa elimu nchini, wakiwamo maofisa elimu wa mikoa na Chama cha Wamiliki wa Vyuo na Shule Binafsi (Tamongsco).
Katika barua hiyo, wizara hiyo imewataka wadau hao kuhakikisha kuwa wanafunzi watakaofeli mtihani huo, wanaendelea na masomo ya kidato cha tatu.
“Matokeo ya kidato cha pili yamepokewa na kufanyiwa uchambuzi ili kupata taswira ya taifa. Taarifa ya matokeo hayo imebaini kuwa watahiniwa waliofanya mtihani na kufaulu ni sawa na asilimia 62 tu,” inaeleza sehemu ya barua hiyo na kuongeza;
“Hali hii inaonyesha kuwa asilimia 31 ya wanafunzi watatakiwa kukariri kidato cha pili, 2014. Wale walioshindwa kwa mara ya pili ambao ni asilimia saba wanatakiwa kuendelea na masomo nje ya mfumo rasmi.”
Barua hiyo inaeleza kuwa wanafunzi waliofaulu kwa wastani wa alama 20 na kuendelea waendelee na masomo ya kidato cha tatu mwaka 2014, wakati awali Serikali ilitoa tamko kuwa watakaoshindwa kufikisha alama 30 watatimuliwa.
“Wanafunzi waliofaulu kwa wastani wa alama 20 hadi 39 wapewe mafunzo rekebishi ‘Remedial class’ wakiwa kidato cha tatu,” inaeleza sehemu ya barua hiyo
SOMA ZAIDI http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/2151230/-/utnth5z/-/index.html.

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LATAJWA

ASHA MIGIRO,NKAMIA NA SAADA WAULA,NCHIMBI,KAGASHEKI NJE, MAGUFULI APETA

Katibu kiongozi wa Serikali ya Tanzania oOmbeni Sefue kwa niaba ya rais Kikwete ametangaa baraza jipya la mawaziri.
                                         
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UHAMISHO NA UTEUZI WA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
______________________________________________
            Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:-
1.0              OFISI YA RAIS
Hakuna mabadiliko.
2.0              OFISI YA MAKAMU WA RAIS
2.1  Waziri wa Nchi (Muungano) - Hakuna mabadiliko
2.2   Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb)
            Waziri wa Nchi (Mazingira).
2.3    Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)
                                                Naibu Waziri                            
3.0              OFISI YA WAZIRI MKUU
Hakuna mabadiliko
            4.0       WIZARA
           
                        4.1  WIZARA YA FEDHA
4.1.1        Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb)
            Waziri wa Fedha
                                    Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)           
                        Naibu Waziri wa Fedha
4.1.2        Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)
                                                Naibu Waziri wa Fedha
                       
4.2              WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Hakuna mabadiliko
           
4.3       WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
4.3.1    Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)
                        Waziri wa Katiba na Sheria
4.3.2        Naibu Waziri - Hakuna mabadiliko
4.4      WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Hakuna mabadiliko
            4.5       WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
           
4.5.1    Waziri - Hakuna mabadiliko
4.5.2    Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb)
                                                Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
            4.6       WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
            Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)
                                                Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
           
4.7        WIZARA YA UJENZI
Hakuna mabadiliko
4.8       WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
4.8.1    Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)
                        Waziri wa Mambo ya Ndani
                       
4.8.2        Naibu Waziri - Hakuna Mabadiliko
           

4.9       WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
4.9.1        Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
4.9.2        Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
4.10     WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
4.10.1  Waziri:  Hakuna mabadiliko
4.10.2  Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb)
                                                Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
14.11   WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
14.11.1  Waziri: Hakuna mabadiliko
14. 11.2 Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
14.12  WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
14.12.1 Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb)
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
14.12.2 Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
14.13      WIZARA YA KAZI NA AJIRA
Hakuna mabadiliko
                                                              
14.14      WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Hakuna mabadiliko
14.15   WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
14.15.1  Waziri - Hakuna mabadiliko
14.15.2  Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
14.16   WIZARA YA MAJI
14.16.1  Waziri - Hakuna mabadiliko
14.16.2  Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)
Naibu Waziri wa Maji
14.17  WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA
14.17.1  Waziri - Hakuna mabadiliko
            14.17.2   Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb)
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
            4.18     WIZARA YA UCHUKUZI
            Hakuna mabadiliko
4.19     WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
4.19.1  Waziri -  Hakuna mabadiliko
4.19.2  Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb)
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
4.20     WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
4.20.1 Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)
Waziri wa Maliasili na Utalii
                        4.20.2 Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)
                                                Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
4.21     WIZARA YA NISHATI NA MADINI
4.21.1    Waziri - Hakuna mabadiliko
4.21.2    Naibu Waziri (Madini) - Hakuna mabadiliko
4.21.3  Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)
Naibu Waziri (Nishati)
     

Balozi Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI
Ikulu
DAR ES SALAAM
19 Januari, 2014

Wednesday, 15 January 2014

Kuhamia teknolojia ya digitali Kenya bado changamoto

Raia wa Kenya bado wana hofu na mchanganyiko wa kuhama kutoka matumizi ya teknolojia ya utangazaji ya analojia na kuhamia teknolojia ya digitali.
Kuingia teknolojia ya digitali Kenya ni kitendawili. Kuingia teknolojia ya digitali Kenya ni kitendawili.
Ifikapo mwaka 2015, muda ambao umepangwa na Umoja wa Mawasiliano ya Kimataifa Duniani kutawsitisha utangazaji wa kutumia analojia. Kuhamia teknolojia ya digitali kunalenga kuwapa huduma bora watumiaji, ingawa kwa nchi za Afrika Mashariki zoezi hilo limekuwa gumu na hivyo serikali husika kulazimika kuahirisha mara kadhaa.
Huku kesi ya kupinga uamuzi wa serikali wa kuvikatalia leseni ya matumizi ya digitali vyombo vya habari nchini Kenya haijamalizika, kesi ambayo ilifunguliwa na wamiliki wa vyombo vikuu vya habari nchini humo bado kuna masuala yaliyoibuka juu ya kuhamia tekenolojia ya digitali, ikiwa ni pamoja na malalamiko juu ya wachina kuchukua fursa kubwa ya kutawala vyombo vya habari, hasa kuelekea teknolojia ya digitali.
Lakini kwa Javas Bigambo, mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Kenya, aliyebobea katika masuala ya vyombo vya habari , utawala na sera ameliambia shirika la habari la IPS kuwa halikuwa suala la bahati mbaya kwa serikali kuipa leseni ya digitali kampuni ya Kichina na kuwanyima wazawa, huku miundo mbinu ya kuanza kutumia digitali ikiwa bado haijatengenezwa.
Anasema mchambuzi huyo na hapa namnukuu "ikiwa bado tuna majonzi ya uamuzi wa Bunge kupitisha muswada tata kuhusu vyombo vya habari nchini humo wenye lengo la kudhibiti tasnia ya uandishi habari nchini bado serikali inaendelea kuyumbisha uhuru wa vyombo vya habari kwa hali ya juu", mwisho wa kumnukuu.
Walalamikia kampuni ya Kichina kupewa leseni
Kwa leseni hiyo, kampuni ya Kichina inayomilikiwa na mtandao wa Pan-Afrika –PANG na SIGNET-shirika la kimataifa la utangazaji , watakuwa na jukumu la kuwaunganisha watumiaji wa televisheni na televisheni hizo , ambapo pande zote zitahusika katika kurusha matangazo kwa makubaliano maalum na wamiliki wa vyombo vya habari, ambapo televisheni za ndani zitawajibika katika kutayarisha matangazo pekee.
Kwa upande wake Alex Gakuru ambaye ni mwenyekiti wa chama cha watumiaji wa mawasiliano ya teknolojia nchini Kenya na mjumbe wa kamati ya kusimamia uhamiaji kutoka analojia kwenda digitali amesema kumekuwa na hali ya wasi wasi kuwa kampuni hiyo ya kichina itadhibiti vyombo vya ndani vya habari na hivyo kudharau katiba na sheria za nchi, ingawa anasema hofu hizo zinapata ushawishi mbaya.
Amesema mawasiliano kwa umma ni suala la kisheria kwa mamlaka za mawasiliano na vyombo vya habari na kwamba kampuni hiyo ya kichina itakuwa na mamlaka ya kusambaza ving'amuzi vyenye kuonyesha chaneli zote cha televisheni za ndani na si kupendelea chaneli fulani,ikiwa itafanya hivyo itajiweka katika hatari ya kufungiwa leseni yake.
Grace Githaiga mdau wa mtandao wa mawasiliano ya teknolojia Kenya anasema kuwa ingawa kamisheni ya mawasiliano Kenya na mamlaka inayosimamia mawasiliao wamedai kuwa vyombo vya habari vya ndani hawakupata zabuni ya leseni ya digitali, hata hivyo vyombo hivyo vina kila sababu ya kulalamikia usimamizi wa kampuni ya kigeni wa digitali kwa kuwa wanaona wamevunjiwa haki yao.
Kampuni ya Kichina yalalamikiwa kupewa leseni. Kampuni ya Kichina yalalamikiwa kupewa leseni.
Hata hivyo amasema wasi wasi juu ya kampuni hiyo ya Kichina kupewa leseni limetiwa chumvi kutokana na ukweli kwamba makamupni ya simu yanatumia tekenolojia ya kichina huku mamilioni ya watu wakiendelea kutumia vifaa vya umeme vinavyotengezwa au kununuliwa kutoka China.
Takwimu zilizotolewa na serikali zinaonyesha kuwa, shirika la habari la utangazaji la China, Xinhua husambazwa habari kwa watu milioni 17 wanaotumia simu nchini Kenya.
Lengo la teknolojia ya Digitali inayoendelea kuhimizwa kutumiwa katika ukanda wa Afrika Mashariki ni kutaka kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano kote duniani.
Teknolojia ya digitali kuongeza ubora
Miongoni mwa faida za kutumia teknolojia ya digitali ni kuongezeka kwa ubora wa matangazo, ongezeko la chaneli za televisheni litakalotokana na matumizi bora ya masafa, kuwepo kwa masafa ya ziada yatakayopatikana baada ya kuzimwa kwa mitambo ya analojia inayotumia masafa mengi.
Faida nyingine zilizobainishwa ni kuongezeka kwa watoa huduma wa mawasiliamo ya simu, matangazo ya televisheni kupatikana kwa vifaa vingi zaidi vya mawasilino kama vile simu za mkononi na kompyuta kupitia mtandao wa internet.
Mwandishi: Flora Nzema/IPS
Mhariri: Mohamed Khelef
Chanzo: dw.de

Tuesday, 14 January 2014

Je, unajua Kila unapofungua website au blog unaacha fingerprints? Ina madhara hivyo jifunnze kujihami


Huwezi kutumia internet kwa matumizi ya kawaida bila kutumia Web browser. Hii ni interface inayotuwezesha kufungua blog, websites na progams nyingine za Internet.  Kuna aina sita za Web browser:
·         Internet ExplorerMicrosoft Inc
·         Google ChromeGoogle Inc
·         Mozilla FirefoxMozilla Corporation
·         Safari Apple
·         Opera Opera Software
Ili kurahisisha matumizi yake, Internet browser zote zinahifadhi kumbukumbu ya web sites zote ulizotembelea. Zinafanya hivyo kwa sababu kadhaa. Sababu ya kwanza ni kwamba kwa kuhifadhi kumbukumbu hizo huwa inamrahisishia mtumiaji anapotaka kutembelea website hizo hizo hapo baadaye. Hii inapelekea internet experience kuwa faster kwa sababu baadhi ya information imehifadhiwa kwenye komputa yako na sio kwenye server maili kadhaa kutoka ulipo.
Pamoja na kwamba web browser inaokoa muda wako, kuna mswala kadhaa yanayoweza kuleta madhara kwenye komputa yako.
Kawanza kumbuka kwa kuwa wewe umerahisishiwa  unapotembelea web sites ulizozea, hali hii inamwezesha mtu mwingine kuziona kumbukumbu hizo zinazohifadhiwa na webbrowser. Baadhi ya web site ulizotembelea inawezekana information zilizohifadhiwa ni muhimu au za siri (kama mambo ya kiakazi). Mtu mwingine mwenye nia mbaya anaweza kujua kila website uliyotembelea na nini ulichofanya kwenye website hiyo. Kuepusha watu kuona information zako usiache fingerprint unapotumia internet. Unafanya hivyo kwa kufuta (delete) kumbukumbu zote ambazo web browser imezihifadhi.
Unaweza kufuta kumbukumbu hizo kirahisi kabisa kama ifuatavyo:
·         Google Chrome: Select “Tools” and choose “Clear Browsing History”
·         Safari: Click on the “History” tab in your menu bar. Select “Clear History” located at the bottom of the list.
·         Internet Explorer: Select the “Safety” drop down menu at the top right of the screen. Choose “Delete Browsing History.”
·         Mozilla Firefox: Click on the “Tools” menu, then select “Clear Recent History.”
Pia kuna njia nyingine unayoweza kutumia web browser bila kuacha fingerprint. Web browser zote zina feature inayokuwezesha kufanya hivyo: Kwa watumiaji wa Internet explore hii inaitwa “In Private”; kwa Mozilla Firefox na Safari hii inaitwa “Private Browsing”; na kwa Google Chrome hii inaitwa “incognito”. Njia hii ni nzuri zaidi hasa kwa wale wanaotumia komputa za public kwa mfano café, shuleni, vyuoni, kazini, n.k.
Kila la kheri
CHANZO: http://it4dev.blogspot.com