m

"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "

-- Dale Carnegie, motivational expert

Sunday, 30 June 2013

MAHAFALI YA KWANZA CASFETA TAYOMI CHUO KIKUU ST.JOHN'S DSM YAFANA

Hatimaye mahafali kwanza ya CASFETA Chuo Kikuu St. John's-Dar es Salaam yamefanyika Jumamosi, tar 29.06.2013 ukumbi wa Mary Peake. Mahafali hayo yalikuwa kwa ajili kuwaaga wahitimu wa shahada ya kwanza ya sanaa na elimu, biashara, uchumi na theolojia. Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa Ndg Christopher Ngubiageya Katibu (M) Vyuo Vikuu (CCM). Mgeni rasmi pamoja na mambo mengina alisisitiza juu ya kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa lakini pia umuhimu wa vijana kushiriki katika siasa na uongozi ili kujenga taifa, kuhubiri amani na utulivu hasa ktika kipindi ambacho Taifa linapita katika misukosuko ya gesi na mabomu.
Picha katika mahafali hayo jinsi yalivyofana;















Picha zote zimepigwa na Dany kwa hisani ya Kapagi Info Institute

Tuesday, 25 June 2013

Tsvangirai apingana na Mugabe kuhusu uchaguzi


Waziri mkuu Morgan Tsvangirai
Waziri mkuu nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai ametoa wito kwa mahakama ya kikatiba nchini humo kufutilia mbali agizo la rais wa taifa hilo Robert Mugabe kuandaa uchaguzi mwishoni mwa mwezi Julai.
Tsvangirai ameonya kuwa huenda taifa hilo likakumbwa na hali ya switofahamu iwapo uchaguzi huo utafanyika.
Katika ombi lake waziri huyo anasema kuwa mda uliotolewa kuandaa shughuli ya usajili wa wapiga kura na uteuzi wa wagombea ni mchache mno.
Hata hivyo Tsvangirai hakusema ni lini angependa uchaguzi huo ufanyike.
Tayari uamuzi huo wa Mugabe kuitisha uchaguzi mapema kuliko ilivyotarajiwa, umekashifiwa na viongozi wengine wa mataifa ya Afrika Kusini.
Rais Mugabe alikwenda mahakamani mwezi jana kufuatia shinikizo kutoka kwa muungano wa nchi za Afrika Kusini (SADC) kubana hatua ya kuakhirisha shughuli nzima ya uchaguzi.
Ikiwa Tsvangirai atashinda kesi hii, anasema mahakamana itakuwa imezuia jambo lisilo la kisheria kuweza kutumbukiza nchi katika hali ya switofahamu.
Tsvangirai anataka uchaguzi ufanyike tu baada ya mageuzi ya sheria za uchaguzi ambayo yametokana na katiba mpya.
bbcswahili.com

Sunday, 23 June 2013

Ajabu; Gari lililomsafirisha Mandela liliharibika

Mandela akiwa na Mkewe Graca
Gari la wagongwa lililokuwa likimsafirisha hospitalini rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela wiki mbili zilizopita, liliharibika likiwa njiani kwenda hospitalini.
Msemaji wa rais wa Afrika Kusini Mac Maharaj, amethibitisha kuwa gari hilo lilikumba na matatizo na kuwa ilibidi rais huyo wa zamani kuhamishwa hadi gari lingine.
Hata hivyo Bwana Maharaj, amesema tukio hilo halikuwa na tishio lolote kwa afya ya Bwana Mandela, kwa sababu alikuwa na madaktari wa kutosha.
Shirika la habari la Marekani CBS limenukuu vyanzo kadhaa vikidai kuwa Mandela alisalia katika eneo hilo kwa zaidi ya dakika arubaini kabla ya usaidizi kufika.
Shirika hilo la CBS limesema kuwa wakati Bwana Mandela alipokuwa akihamishwa hadi gari lingine viwango vya joto vilikuwa chini sana.
Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alikuwa akisafirishwa kutoka hospitali moja mjini Johannesburg hadi Pretoria, wakati wa tukio hilo lililotokea tarehe nane Juni mwaka huu.
Mandela alilazwa hospitalini huku hali yake ikiwa mbaya kutokana na maambukizi ya mapafu ya mara kwa mara na tangu wakati huo amekuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Hii ni mara ya tatu kwa Bwana Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.
Chanzo; BBC

Rais Kagame afanya mabadiliko ya jeshi


Rais Kagame wa Rwanda
Rais Kagame wa Rwanda

Rais Kagame afanya mabadiliko kwenye uongozi mkuu wa jeshi na kumteua Jenerali Patrick Nyamvumba kuwa mkuu mpya wa majeshi.

Jenerali Patrick Nyamvumba amechukua nafasi ya jenerali Charles Kayonga aliyeshikilia nafasi hiyo tangu mwaka 2002.
Mkuu mpya wa majeshi ya Rwanda,alikuwa kamanda wa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda amani UNAMID katika jimbo la Darfur nchini Sudan tangu mwaka 2009.
Mabadiliko hayo pia yameshuhudia wadhifa mpya katika uongozi wa jeshi la Rwanda, ambao ni wadhifa wa mkaguzi mkuu wa jeshi uliopewa Brigedia jenerali Jack Nziza baada ya kupandishwa cheo na kuwa meja jenerali.Jack Nziza amekuwa akihudumu kama mkurugenzi mkuu katika wizara ya ulinzi.Pia mkuu wa zamani wa idara ya upelelezi wa nje kanali Dany Munyuza ameteuliwa kuwa naibu kamishna mkuu wa polisi ya Rwanda.Sababu za mabadiliko hayo hazijawekwa wazi.
Chanzo; BBC

Jasusi Snowden atua Moscow

Edward Snowden

Ndege iliyombeba mtaalamu wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani, Edward Snowden imetua mjini Moscow baada ya kusafiri kutoka Hong Kong.

Chanzo kutoka ndege hiyo ya taifa la Urusi kimesema bwan snowden anayetakiwa na Marekani kwa mashtaka ya wizi wa siri za serikali,
Amepanga kuondoka hapo kesho jumatatu kuelekea nchini Cuba kabla ya kuelekea Venezuela ambako amepanga kuomba hifadhi.
Mamlaka ya Hong Kong imesema bwana Snowden aliondoka kwa hiyari yake mwenyewe na kisheria baada ya kugundua njama za kutaka kumkamata zinazofanywa na mtandao wa kijasusi wa marekani kambi ya Uchina.
Hong Kong imesema imeyakataa maombi ya marekani ya kutaka kumkamata na kumrejesha bwana Snowden nchini Marekani kwa nguvu kwa kuwa maombi hayo hayaendani na sheria za ndani za nchi hiyo.
Chanzo; bbcswahili.com

Friday, 21 June 2013

Kesi dhidi ya Rais Kenyatta yaakhirishwa


Rais Uhuru Kenyatta
Mahama ya kimataifa ya ICC imeakhirisha siku ya kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya rais Uhuru Kenyatta hadi tarehe 12 mwezi Novemba mwaka huu.
Hii ni kufuatia ombi la mawakili wa Rais Kenyatta kutaka kesi yao kuahirishwa hadi mwezi Januari mwaka ujao.
Mahakama iliamua kuwa upande wa Kenyatta unahitaji muda wa ziada ili kujiandaa ipasavyo kwa kesi, kwa sababu viongozi wa mashtaka walichelewa kufichua ushahidi walio nao dhidi ya rais Kenyatta.
Kenyatta anakabiliwa na tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadmau wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya miaka sita iliyopita, akisemekana kuunga mkono mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya watu wa kabila moja.
Naibu Rais wa Kenya William Ruto naye pia anakabiliwa na kesi katika mahakama ya ICC kuhusu tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kupanga mashambulizi dhidi ya jamii hasimu.
Majaji waliwaalika mawakili wa Uhuru Kenyatta kutoa maoni yao kuhusu muda wanaotaka ili kujiandaa kwa kesi dhidi ya mteja wao.
Baada ya kupokea maoni kutoka kwa upande wa utetezi, upande wa mashtaka, pamoja na waakilishi wa kisheria, majaji waliamua kuakhirisha kesi hiyo kutoka tarehe 9 Julai mwaka huu hadi Novemba.
Tarahe hiyo mpya ilifikiwa baada ya kuzingatia maswala mbali mbali ikiwemo haja ya upande wa mashtaka kujiandaa vyema kwa utetezi wao na mipango ya usafiri.
Rais Kenyatta ameshtakiwa kwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya , makosa ya jinai ikiwemo, mauaji, kuwahamisha watu kinyume na sheria, ubakaji , mateso na vitendi vingine vya kinyama vinavyodaiwa kufanywa wakati wa ghasia hizo mwaka 2007/2008

Mazingira mabaya shuleni hukimbiza walimu

MWALIMU ni mtu wa muhimu katika jamii yoyote kwa kuwa anabadilisha maisha ya kila mtu kutoka hatua moja kwenda nyingine. Cha kushanganza maisha yake ni tofauti na kazi kubwa anayoifanya. Pia wanapata changamoto nyingi katika utendaji kazi wao… wengine wanajikuta wakivikimbia vituo vyao vya kazi kutokana na mazingira magumu wanayofanyia kazi.

Jambo la kusikitisha walimu wanafikia hatua ya kutembea kilomita kubwa kutoka majumbani kwao kwenda kwenye vituo vyao vya kazi hali ambayo haiwezi kuleta matokeo mazuri ya elimu nchini.

Mwalimu anatembea kila siku kilometa 10 kwenda na kurudi kutoka shuleni, anafika amechoka na hana hamu ya kufundisha hivyo anafundisha chini ya kiwango kinachotakiwa.

Licha ya Serikali kujitahidi kuajiri walimu wengi kwenye vituo mbalimbali karibu mikoa yote ya Tanzania, bado imesahau kuwa baada ya kutoa ajira walimu wanaenda kukaa katika mazingira gani.

Idadi kubwa ya walimu wanapelekwa maeneo ya vijijini kutokana na uhaba wa walimu katika maeneo hayo, lakini huduma za kukidhi mahitaji yao bado ni hafifu.

Inasikitisha kuwaona walimu ambao ni mhimili mkubwa katika jamii wanalala jikoni kwa miaka mitatu huku wafanyakazi wengine wakiwa wanatembea zaidi ya kilomita kumi, jambo hili linasikitisha na linatia aibu kwa Serikali yetu.

Kuhusu walimu wanaotoroka kazini na kujiunga na vyuo vya elimu ya juu pasipo ridhaa ya mwajiri, tatizo hili linaathiri zaidi mikoa iliyopo Kanda ya Ziwa na Kaskazini, ambayo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu ambapo chanzo kikubwa ni mazingira mabaya ya kufanyia kazi.

Taratibu za kuyarekebisha maisha ya walimu yatasaidia kupunguza utorokaji wa walimu katika maeneo mbalimbali hapa ikiwemo vijijini ambapo matatizo yanakuwa mengi kuliko wale wa mjini.

Walimu wengi hukimbilia mjini ili kukwepa matatizo ya vijijini ambapo baadhi yao wanajikuta wakiishi kwenye nyumba za udongo na kuamua kuachana na kazi ya ualimu na kujihusisha na biashara nyingine.

Kutokana na hali kuwa tete Serikali ilipanga kuwachukulia hatua watumishi wake zaidi 800 waliotoroka kazini na kujiunga na vyuo vya elimu ya juu bila idhini ya mwajiri.

Jumla ya walimu 26,537 wameajiriwa serikalini kwa mwaka wa fedha 2012/2013, walimu wa ngazi ya cheti walioajiriwa ni 13,568.

Kati yao walimu 13,527 wamepangwa kufanya kazi katika shule za msingi zilizopo kwenye halmashauri na walimu 41 wamepangwa katika shule za msingi za mazoezi zilizo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Jumla ya walimu wa sekondari na vyuo vya ualimu walioajiriwa ni 12,973 wakiwemo walimu wa Shahada 8,887 na Stashahada 4,086, lakini swali la kujuuliza maeneo waliyopangiwa yanakidhi viwango?

Idadi ya walimu walioajiriwa mwaka 2012/2013 imeongezeka kwa asilimia 11 sawa na walimu 2,630 ikilinganishwa na walimu 23,907 walioajiriwa mwaka uliopita 2011.

Walimu wapya wanakuwa na shauku kubwa ya kuanza kazi, lakini baada ya kuripoti kwenye vituo vyao vya kufanyia kazi na kukuta mazingira si mazuri baadhi yao wanaamua kuondoka baada ya wiki tatu au mwezi mmoja.

Baada ya Serikali kutilia shaka matokeo hayo Baraza la Mitihani Tanzania (BAMITA) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wameamua kurudia kusahihisha lakini matokeo hayajabadilika kwa asilimia kubwa sio siri ufaulu si nzuri kama inavyotakiwa.

Licha ya Serikali kujitahidi kuwaajiri walimu kwa wingi kila mwaka lakini hali bado ni mbaya hasa maeneo ya vijijini ambapo unaweza kuikuta shule ina jumla ya wanafunzi mia 400 lakini wanafundishwa na walimu wawili au watatu hali ambayo haiwezi kuleta matokeo mazuri.

Walimu hawawezi kufanya kazi zao kwa ufanisi ulio juu huku wakiwa wanalala jikoni kwa miaka mitatu na wengine kutembea kwa kilomita kumi,kitu ambacho hakiwezekani.

Wanafunzi wa sasa wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika lakini mwanafunzi huyo anafaulu kwenda kidato cha kwanza,kwa hali hii tusitegemee kupata matokeo mazuri na viongozi wazuri wa baadaye.
Chanzo; Mtanzania.co.tz

Mizengo Pinda: Nasema wapigwe tu

Share bookmark Print Email Rating
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda 
Na Waandishi Wetu  (email the author)

Posted  Alhamisi,Juni20  2013  saa 20:57 PM
Kwa ufupi
Lazima tuwakamate na kama katika kuwakamata watafanya jeuri, jeuri, watapigwa tu kabla ya kupelekwa tunapotakiwa kuwapeleka, kwa sababu hatuwezi kuendelea na hali hii, mkadhani kwamba tutafika tunapokwenda.

Dodoma/Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameagiza vyombo vya dola kuwashughulikia kwa kuwapiga wale watakaokataa kutii amri wakati wakifanya vitendo vya uvunjifu wa amani.
Akizungumza katika Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Hapo kwa Waziri Mkuu, bungeni Dodoma jana, Pinda alisema watu wanapokaidi wanajitakia matatizo na vyombo vya dola.
Alisema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu aliyeuliza: “Serikali ipo tayari kiasi gani kubainisha na kuchukua hatua stahiki, badala ya kusakama makundi fulani, tujue chanzo halisi cha vurugu hizi na matatizo haya na jinsi gani vyombo vya dola vinavyoshughulikia kwa sababu yapo malalamiko katika baadhi ya maeneo kama Mtwara kwamba wananchi wanapigwa na vyombo vya dola?”
Waziri Mkuu alijibu: “Ni lilelile nililosema... mwishowe unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu... hamna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.
“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine... maana tumechoka.”
Pinda alisema Serikali imedhamiria kurejesha amani nchini ikiwamo mkoani Mtwara na kuwataka Watanzania waiache Serikali ifanye kazi hiyo. Alisema Serikali ina orodha ya watu wanaosemekana kuwa ni vyanzo vya vurugu na matatizo yaliyotokea Mtwara na kushangaa wale wanaopinga kukamatwa kwao.
“Lazima tuwakamate na kama katika kuwakamata watafanya jeuri, jeuri, watapigwa tu kabla ya kupelekwa tunapotakiwa kuwapeleka, kwa sababu hatuwezi kuendelea na hali hii, mkadhani kwamba tutafika tunapokwenda. Nami nasema vyombo vya dola vijipange imara vihakikishe vinadhibiti hali hii,” alisema.
Hata hivyo, jibu hilo lilipata upinzani wakati Mbunge wa Konde (CUF), Khatibu Said Haji alipomwuliza Waziri Mkuu: “Hapo awali umetoa kauli nzito ya kuliambia taifa hili kwamba wale raia wote, ambao watakaokuwa wakaidi wapigwe tu na watapigwa tu; naomba ninukuu Katika Ibara ya 13 na Kifungu cha 6B cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
“Ni marufuku kwa mtu yeyote aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kuteswa kama mtu mwenye kosa, mpaka itakapothibitika anayo hatia kwa kutenda kosa hilo.
“Pia ibara hiyohiyo Kifungu cha 6 E; kinasema ni marufuku kwa mtu yoyote, kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazoweza kumdhalilisha. Kwa kauli yako uliyoitoa huoni kwamba umevunja Katiba?” Akijibu swali hilo, Pinda alisema ni lazima kutofautisha kati ya mtu aliyekwishakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria... “Mimi ninayemzungumza hapa ni mtu yule ambaye ameamua kufanya vitendo hajakamatwa na ndiyo maana nilikwambia usiandamane... hapa mahali hutakiwi kwenda wewe ukaamua kutumia mabavu kwa sababu mko wengi, ndiyo maana nikasema, hawa watu tutashughulika nao hivyohivyo.”
Mbunge huyo hakuridhishwa na majibu hayo na kumtaka Waziri Mkuu kuyafuta.
Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliingilia katika na kumweleza mbunge huyo kuwa kila mtu alikuwa amemwelewa Waziri Mkuu na hakukuwa na haja ya kuendelea na hoja hiyo.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mizengo-Pinda--Nasema-wapigwe-tu/-/1597296/1889674/-/xk60drz/-/index.html 

Saturday, 8 June 2013

ROHO MTAKATIFU NA KAZI ZAKE KWETU

SOMO LA 1 semina

ROHO MTAKATIFU,MTOA UTAKATIFU
Katika somo la kwanza katika mfululizo wa masomo haya yanayohusu Roho Mtakatifu,Tulijifunza kwamba Roho Mtakatifu,ni mtakatifu,hivyo anakuwepo na kudumu mahali palipo na utakatifu tu.Tukiwana maisha ya uchafu,yaani dhambi;humfanya Roho Mtakatifu akose makao kwetu,na hivyo hawezi kuwepo kwetu.Kama alikuwepo mwanzo kwetu,huondoka (1Samweli 16:14;
Zaburi 51:4,10-11).Sasa swali linakuja,tunawezaje kuwa watakatifu katika maisha yetu ili Roho Mtakatifu afanye makao
kwetu?Jibu ni kwamba,Roho Mtakatifu ,ndiye huyohuyo anayetoa utakatifu tunaouhitaji.Sasa tunamwangalia Roho
Mtakatifu kama Mtoa Utakatifu,kwa kutafakari kazi yake hiyo katika vipengere vitano:-
1. ROHO MTAKATIFU,ROHO ATUPAYE KUZALIWA MARA YA PILI
2. ROHO MTAKATIFU ROHO AWAFUFUAYE WATU WALIOKUFA KIROHO
3. ROHO MTAKATIFU, ROHO AWATIAYE UZIMA WATU WALIOZIMIA KIROHO
4. ROHO MTAKATIFU ROHO ATUPAYE UTAKASO
5. ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE TUNDA LA ROHO

BOFYA HAPA USOME ZAIDI

http://calivarychurch.blogspot.com/2011/04/roho-mtakatifu-na-kazi-zake-kwetu.html 

Roho mtakatifu ni nani?



Swali: "Roho mtakatifu ni nani?"

Jibu:
Kuna utatanishi mwingi juu ya kumtambua Roho mtakatifu. Wengine humchukulia kama nguvu Fulani zisizoonekana. Wengine huamini kwamba ni uwezo wa Mungu ambao Mungu huuachilia maishani mwa wale ambao ni waumini wa kristo. Je, biblia inasemaje juu ya Roho mtakatifu? Kwa kifupi biblia inasema kwamba Roho mtakatifu ni Mungu. Pia biblia inasema kuwa Roho mtakatifu ni mtu, mwenye akili, hisia na mapenzi yake.

Swala la kuwa Roho mtakatifu ni Mungu limo ndani ya aya nyingi za biblia kama vile Matendo 5:3-4. Katika ayah ii petro anapambana na anania aliyemdanganya Roho mtakatifu na nasisitiza yakuwa “hukumdanya mtu bali Mungu.” Hili ni tangazo la wazi kwamba kumdanganya Roho mtakatifu ni kumdanganya Mungu. Tunaweza pia kujua Roho mtakatifu ni Mungu kwa kuwa ana tajwa na hali sawa na za Mungu. Roho mtakatifu yuko kila mahali katika Zaburi 139:7-8, “nitaenda wapi nijifiche na Roho? ama nitakimbilia wapi mbali na uwepo wako? Nikipanda juu mbinguni, huko uko; nikifanya malazi yangu kuzimu, tazama uko huko,” tena katika wakorintho wa Kwanza 2:10 tunaona hali yakuwepo kila mahali kwa Roho mtakatifu “Lakini Mungu ameyajulisha kwetu kupitia Roho wake mtakatifu. Kwa kuwa Roho huyachunguza mambo yote, naam, mambo ya siri ya Mungu. Kwa maana ni nani ayajuaye ya mwanadamu isipokuwa roho ya mwanadamu inayokaa ndani yake? Vivyo hivyo, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.”

Tunaweza kujua kweli kwamba Roho mtakatifu ni Mungu kwa kuwa ana akili, hisia na mapenzi yake. Roho mtakatifu hufikiri na hujua (Wakorintho wa kwanza 2:10). Roho mtakatifu anaweza kuugua (Waefeso 4:30). Roho hutuombea (Warumi 8:26-27). Roho mtakatifu hufanya maamuzi kutokana na mapenzi yake mwenyewe (Wakorintho wa kwanza 12:7-11). Roho mtakatifu ni Mungu, sehemu ya tatu ya utatu wa Mungu. Kama Mungu, Roho mtakatifu anaweza kufanya kazi ya msaidizi na mshauri kama vile Yesu kristo aliyevyoahidi kuwa atakuja kufanya (Yohana 14:16,26; 15:26).
Chanzo; http://www.gotquestions.org/Kiswahili/roho-mtakatifu.html