| Wednesday, 17 October 2012 21:34 |
Waandishi Wetu, Dar na Zanzibar POLISI mkoani Dar es Salaam na wale wa Kisiwani Zanzibar, jana walitumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kusambaratisha makundi ya watu wanaodaiwa kuwa waumini wa Dini ya Kiislamu, waliopanga maandamano kushinikiza kuachiwa kwa viongozi wao. Kisiwani Zanzibar vurugu kubwa ziliibuka baada ya kusambaa taarifa kuwa Kiongozi wa Kundi la Uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed alitekwa nyara juzi saa 3 usiku akiwa kwenye gari lake na dereva wake. Vurugu hizo zilisababisha uharibifu wa mali kadhaa ikiwamo Maskani Kaka ya Kisonge inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo ilichomwa moto na waandamanaji. Waandamanaji hao pia walichoma moto baa za Darajani na Mbawala eneo la Mikunguni na baadhi ya nyumba za kulala wageni, kabla Vikosi vya Kutuliza Ghasia (FFU) na Kikosi cha Zima Moto kudhibiti vurugu hizo kwa mabomu ya kutoa machozi. Pia magari kadhaa yalichomwa moto na kuharibiwa vibaya yakiwa yameegeshwa katika maeneo mbalimbali, huku mipira na matairi vikichomwa katika barabara kadhaa. Katika maeneo ya Mjini baadhi ya njia zilifungwa na watu waliokuwa wakitoka kazini walishindwa kwenda nyumbani. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni yale ya Malindi, Darajani hadi Michenzani ambako njia zilifungwa na mabomu yalisikika yakipigwa mfululizo. Katibu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Sheik Abdallah Said alisema, “Taarifa tulizonazo ni kwamba Sheikh Farid ametoweka katika mazingira ya kutatanisha…Alitoka kwake Mbuyuni katika gari yeye na kijana wake wa hapo nyumbani, lakini baadaye kuna gari ikamfuata na kusimama na ndipo alipoingia katika hilo gari jingine na hakuonekana tena. Hatujui ni kina nani waliomchukua na hatujui ilikuwaje akaingia katika hilo gari ...” Polisi waliimarisha ulinzi katika baadhi ya maeneo hasa Msikiti wa Mbuyuni ambao uko jirani na makazi ya Sheikh Farid. Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema polisi halihusiki na kukamatwa kwa Farid, lakini wao wanaamini kwamba ‘amejipoteza’ mwenyewe na kujificha. Kamishna Mussa alisema polisi watawasaka wote waliosababisha vurugu hizo, na kwamba hadi sasa hawafahamu chanzo chake bado. “Tunafanya uchunguzi zaidi kujua chanzo cha fujo hizo ingawa mimi sijui habari za kutekwa Farid, sasa tunasema tunachunguza chanzo cha vurugu hizo na tukishapata uthibitisho na waliosababisha tutawafikisha mahakamani kujibu mashtaka,” alisema kamishna huyo. Ilivyokuwa Zanzibar Vurugu hizo zilianza katika maeneo mbalimbali muda mfupi baada ya vijana kadhaa kukusanyika katika eneo la Darajani kando ya Soko Kuu majira ya asubuhi, kutokana na kuzagaa kwa taarifa kwamba Sheikh Farid alikuwa haonekani. Idadi ya vijana hao ilikuwa ikiongezeka kadiri muda ulivyosonga, huku wengi wao wakiwa na silaha za aina mbalimbali zikiwamo magongo na mawe, hali iliyoibua hofu kwa wafanyabiashara wa eneo hilo, hivyo baadhi yao waliamua kufunga maduka. Maeneo yalioharibiwa ni pamoja na baadhi ya nyumba za kulala wageni ambazo zimechomwa moto katika eneo la Amani, huku baadhi ya vijana wakionekana wakikimbia na kreti za pombe. Katika eneo la Darajani, vijana kadhaa wakishirikiana na Wamachinga, walionekana wakivunja kisha kuingia katika moja ya maghala ya kuhifadhia bia, ambako walipora bidhaa zote zikiwamo kreti kadhaa za bia zilizokuwa zimehifadhiwa humo. Baadhi ya wenye maduka walifunga na kutoweka, lakini waporaji waliiba baadhi ya bidhaa vikiwamo vyakula, kisha kutokomea navyo kusikojulikana. Katika maeneo ya Ng’ambo ambayo ni Amani, Mikunguni, Kwerekwe na Daraja Bovu vijana walioonekana kuwa na hamasa, waliingia kwenye makazi ya watu na kuiba vitu kadhaa, na kila mabomu yalipopigwa walikimbilia vichochoroni na baada ya muda walirejea tena. Maeneo ya Malindi, Michenzani na Rahaleo, kulikuwa na vurugu za urushaji mawe na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu katika maeneo hayo. Matawi ya miti ilikatwa na kuunganishwa na magari mabovu kuwekwa barabarani kisha kuchomwa moto. Hali hiyo ilisabababisha uharibifu mkubwa katika baadhi ya barabara, na katika fujo hizo baadhi ya vijana walikamatwa. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Azizi Juma Mohammed alithibitisha kutokea kwa fujo hizo na kusema Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kujua chanzo chake na taarifa kamili zitatolewa baada ya kukamilika uchunguzi huo. Ponda Dar Jijini Dar es Salaam, baadhi ya watu walipanga kufanya maandamano hadi Makao Makuu ya Polisi, kupinga kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyekamatwa juzi usiku na kushikiliwa kutwa nzima ya jana katika Kituo Kikuu cha Polisi. Ponda alitiwa mbaroni kwa tuhuma za kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani jijini Dar es Salaam, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisisitiza kuwa polisi wamechoka kuvumilia harakati zake za kutaka “nchi isitawalike”. “Kuanzia leo uvumilivu kwa Jeshi la Polisi dhidi ya watu wasiofuata sheria za nchi umekwisha. Kwa kuwa Ponda ni mtu anayepotosha watu waliopo chini yake wanaotaka kuandamana bila utaratibu wasitulaumu kwa lolote lile litakalotokea,” alisema Kova. Kova alisema hadi jana Ponda alikuwa bado anahojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Mkoa wa Dar es Salaam na kwamba ushahidi ukijitosheleza, atafikishwa mahakamani wakati wowote. Alisema taasisi anayoingoza Sheikh Ponda haijasajiliwa kwa mujibu wa sheria kufanya shughuli za dini. Hivyo basi shughuli zote zinazoendesha na taasisi hiyo si halali. "Natoa wito pia kwa wafuasi wa kiongozi huyo, walioshiriki katika vurugu mbalimbali za hivi karibuni, wajisalimishe haraka kwa kuwa sasa tupo katika mchakato wa kuwasaka, kuwakamata na baadaye kuwafikisha mbele ya sheria," alisema. Tuhuma za Ponda Kamanda Kova alidai kuwa Sheikh Ponda amekuwa akichochea vurugu na kuwashawishi wafuasi wake kuidharau Serikali na vyombo vya usalama. “Ponda amekuwa ni mtu ambaye amefanya nchi hii, hasa katika Jiji la Dar es Salaam kukaa katika hali ya wasiwasi. Ijumaa imekuwa siku ya fujo badala ya kuwa siku ya amani,” alisema Kova. Alisema vurugu hizo zinazoongozwa na Sheikh Ponda zimekuwa zikisababisha baadhi ya watu kushindwa kwenda kazini siku za Ijumaa na hali hiyo haivumiliki tena. Kamanda Kova alitaja tuhuma nyingine dhidi ya Sheikh Ponda kuwa ni kuongoza kundi la watu kwenda kuvamia kiwanja namba 311/3/4 eneo la Chang’ombe ambacho kinamilikiwa na kampuni Agritanza. "Kiwanja alichokwenda kukivamia kilikuwa mali ya Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata) na kiliuzwa kihalali kwa kampuni hiyo," alisena. Alitaja tuhuma nyingine kuwa ni kufanya maandamano kinyume cha sheria, ikiwamo kuweka kambi Makao Makuu ya Polisi bila kibali cha jeshi hilo wiki kadhaa zilizopita. Kamanda huyo alisema Ponda anashikiliwa pia kwa kuwa mstari wa mbele kupambana na vyombo vya dola na Serikali, ikiwa ni pamoja na kushawishi wafuasi wake kumdharau Rais wa nchi. “Vilevile amekuwa akiendesha maandamano na kukusanyika Kiwanja cha Kidongo Chekundu, huku wakijitapa kuwa wana nguvu zaidi ya Jeshi la Polisi,” alieleza Kova. Polisi pia wanamtuhumu Ponda kwa kuanzisha vurugu na vitisho dhidi ya Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Mufti Shaaban Bin Simba na kutaka kumtoa madarakani kwa nguvu pamoja na kutaka kuvamia ofisi yake. Alikamatwaje? Kamanda Kova alisema Ponda alikamatwa na askari waliomuwekea mtego kutokana na yeye kuwa bingwa wa kutoroka kila akifanya matukio. “Askari waliowekwa maalumu kwa ajili ya kumkamata walifanikiwa kumtia nguvuni saa 4:00 usiku karibu na eneo la maficho yake ambako alipelekwa na pikipiki,” alisema Kova. “Hivi Ponda ni nani mpaka awe na uwezo wa kumpa Rais aliyechaguliwa na wananchi siku saba kuwaachia watu waliopo mahakamani yeye amechaguliwa na nani kuongoza taasisi aliyonayo na anatoa wapi nguvu za kufanya mambo yote hayo?,” alihoji Kova. Alisema kulingana na matukio anayoyaongoza Ponda, wananchi wameanza kuona kama anaogopwa na vyombo vya dola, jambo ambalo siyo kweli. Aliongeza kuwa polisi wana uwezo wa kumdhibiti, isipokuwa walikuwa wanatumia busara tangu alipoanza vurugu na kwa sasa uvumilivu umewashinda, hivyo wataanza kumshughulikia. Vurugu zazuka Kukamatwa kwa Sheikh Ponda kulizua vurugu jijini Dar es Salaam na kufanya baadhi ya wakazi wake hasa maeneo ya Mnazi Mmoja na Kariakoo, kuingiwa kiwewe baada ya polisi kutumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha ili kuwasambaratisha watu waliokuwa wanataka kuandamana kwa lengo la kushinikiza kiongozi huyo aachiwe. Hali hiyo ilisababisha watu kukimbia ovyo katikati ya iji na kuongezeka kwa misongamano ya magari, jambo lililofanya usafiri wa daladala kuwa mgumu kwenda na kutoka katikati ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyabiashara walifunga maduka yao wakihofia kuporwa mali wakati wa vurugu hizo, baada ya vibaka kujichanganya wakijaribu kufanya uhalifu huo. Katika eneo la Mnazi Mmoja, polisi walirusha maji ya kuwasha kusambaratisha kundi la watu hao, huku wengine wakiwa wanadhibitiwa walipokuwa wakienda Makao Makuu ya Polisi ili kumtoa kiongozi huyo. Baadhi ya mashuhuda walisema, mbali na Ponda watu hao walikuwa wanataka kwenda polisi kuwatoa watu waliokuwa wanashikiliwa kituoni hapo kwa tuhuma za kufanya vurugu na kuharibu makanisa katika Kata ya Mbagala wilayani Temeke. Imeandikwa na Salma Said, Zanzibar, Zaina Malongo na Festo Polea, Dar. E&P Chanzo: Mwananchi |
m
"If you want to conquer fear, don't sit at home and think about it. Go out and get busy. "
-- Dale Carnegie, motivational expert
Thursday, 18 October 2012
VURUGU ZA UAMSHO ZANZIBAR NA SHEHE PONDA AKAMATWA
Tuesday, 16 October 2012
TAKWIMU ZA UCHOMAJI MAKANISA TANZANIA NA TAMKO LA TAG
TAKWIMU ZAONYESHA TANGU MWAKA 1985-2012 MAKANISA 46 YAMECHOMWA ,KUBOMOLEWA NCHINI
![]() |
| Askofu David Mwasota. |
Imeelezwa
kuwa tangu kuibuka kwa wimbi la uchomaji
wa makanisa linalofanywa na watu
wanaoaminika kuwa wanaharakati wa
Kiislamu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeyakumba zaidi ya
makanisa 46.
Hayo
yameelezwa na Katibu Mkuu wa Baraza la
Maaskofu wa Kipentekoste nchini Tanzania (PCT) Askofu David Mwasota wakati
akizungumza na Gazeti Msemakweli akiwa Kisiwani Zanzibar.
Kiongozi
huyo alikuwa mmoja wa wajumbe wa mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini
ya Kikristo, viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)na makamanda
wakuu wa jeshi la Polisi ambapo ulijadili kwa kina juu ya vurugu zilizotokea
visiwani Zanzibar.
Kwa
mujibu ya Mwenyejiti wa kundi linaloendesha mihadhara ya Kikristo
inayosahihisha upotoshwaji wa Maandiko Matakatifu ya Biblia unaofanywa na
Wahadhiri wa Kiislamu Mwinjilisti Cecil Simbaulanga, takwimu zinaonesha kwamba makanisa yaliyoteketezwa na Waislamu tangu
mwaka 1985 visiwani Zanzibar pekee ni
26, huku Tanzania Bara yakifikia 20.
Askofu
Mwasota alisema hadi mapema wiki
iliyopita wanaharakati wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu
Zanzibar(JUMIKI) walipofanya vuruguru na kuchoma moto makanisa kisiwani Zanzibar, viongozi wa
Kikristo wamekuwa wakitoa taarifa za
uhalifu dhidi ya makanisa na nyumba za wachungaji, lakini hakuna hatua
zilizochukuliwa.
Katika
mahojiano kwa njia ya simu na Msemakweli, Askofu Mwasota alisema kutokana na
hilo, viongozi wa Kikristo waliokutana na viongozi wa SMZ katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Kariakoo
lililochomwa moto, alisema kimsingi viongozi hao kupitia Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bwana Mohammed Aboud Mohammed, waliahidi kuyalinda makanisa dhidi ya Waislamu
wakorofi.
''Angalau
kauli kama hiyo imetupa moyo na
kuturidhisha kwa vile haikuwepo siku za nyuma na kweli tunashuhudia ulinzi umeimrishwa makanisani”, alisema Askofu
huyo wakati akihojiwa na Msemakweli kwa njia ya simu kutoka Zanzibar.
Alisema
tayari watu 30 wamekamatwa kuhusiana na vurugu hizo.
Hata
hivyo alipoulizwa nini serikali inasema
kilikuwa chanzo cha vurugu hizo, alisema bado uchunguzi unaendelea na
kwamba si vyema kukurupuka na kutaja
chanzo hicho kabla ya uchunguzi makini kufanyika.
Kwa
upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani Dakta Emanuel Nchimbi aliyeshiriki katika
mkutano huo, alionya kuwa suala la amani
na ulinzi wa raia na mali zao halina
mjadala na kuvitahadharisha vikundi vinavyohatarisha amani na kwamba vitapambana na mkono wa Dola.
Mei
26 na 27 mwaka huu, vurugu kubwa zilitokea kisiwani Zanzibar
baada ya wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu
Zanzibar (JUMIKI), kushinikiza Jeshi la Polisi limuachie kiongozi wao
Sheikh Mussa Issa ambaye alikamatwa.
Baada
ya wafuasi hao kushindwa kuvamia kituo cha Polisi Madema, kufuatia Askari wa
FFU kuwatawanya kwa mabomu ya machozi, waliamua kuingia mitaani na kufanya
kitendo cha kushangaza cha kuharibu mali za makanisa mawili na
kuyachoma moto.
Katika
kile kinachooneka kuwa nyuma ya vurugu
hizo kuna mkono wa udini na siasa, licha ya wafuasi wa JUMIKI kuchoma moto
makanisa, pia walikuwa wakiwasaka watu kutoka Tanzania Bara huku wakitamka kwamba hawautaki muungano.
Wakati
kanisa
la TAG lilichomwa moto Mei 27 mwaka huu, Porikia ya Kanisa Katoliki
Mpandae iliripotiwa kuchomwa moto mchana wa Mei 28 mwaka huu na kundi
la
wafuasi wa JUMIKI lililokuwa likitoka katika Mahakama ya Mwanakwerekwe
kusikiliza kesi ya wenzao waliokamatwa kwa kuhusika na vurugu hizo.
Kati
ya watu 30 waliokamatwa na kufikishwa mahakamani wamo viongozi watatu wa JUMIKI akiwemo mkuu wake
Sheikh Mussa Juma Issa, ambapo wanatuhumiwa
kukusanyika kinyume na sheria na kufanya fujo. Watuhumiwa hao hata hivyo wako
nje kwa dhamana.
Naye
Mwenyekiti wa Kundi la Biblia ni Jibu nchini Tanzania
ambalo ni maarufu kwa kupigania imani ya Kikristo dhidi ya upotoshwaji unaofanywa
na Wahadhiri wa Kiislamu Cecil Simbaulanga aliliambia Msemakweli kuwa vurugu
za Zanzibar ni
za kidini dhidi ya Ukristo.
“Ndio
maana waliohusika ni nazo ni Mashehe wanaoeneza chuki dhidi ya Ukristo. Haya yote
nilishayaeleza katika katika kitabu
changu kinachozungumzia Mchango wa Kanisa katika miaka hamsini ya Uhuru, ambapo
katika ukurasa wa 36 niliitaka serikali kuchukua hatua za kudhibiti wimbi la
uchomaji makanisa”, alisema Simbaulanga.
Alisema
kwa kilichotokea sasa anaitaka serikali
ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar ifidie makanisa sita yaliyochomwa moto
katika vurugu za sasa kutokana na uzembe
wake na kutosikiliza hoja za maana.
“Unajua
haiingii akilini kwamba Waislamu Zanzibar ambao ni asilimia 99.9 inakuwaje
walalimikie mfumo Kristo”, alisema Mwinjilisti Simbaulanga na kubainisha kuwa
kinachofanyika ni mbinu tu za kusambaza chuki ili kuua Ukristo Zanzibar.
Alisema
kwa hali ilivyo sasa ni lazima SMZ iache kufundisha watoto Uislamu pekee
katika shule za msingi kama inavyofanya sasa, Kama
kweli inataka haki itendeke.
Mwinjilisti
Simbaulanga alilitaka Jeshi la Polisi na SMZ kutopotosha ukweli kwamba
wanaofanya vurugu za uchomaji moto makanisa ni wahuni bali waeleze ukweli
kwamba ni Waislamu.
“Haya
mambo sisi tunajua. Tunazo DVD za wote waliopanga mambo haya kuanzia mwanzoni
mwa mwaka huu, kama
ushahidi mzito na tunawajua. Tuko tayari kutoa ushahidi huo.Hawa sio wahuni ni
viongozi wa wanaharakati wa Kiislamu wanaofahamika wazi”, alisisitiza
Simbaulanga.
Akizungumza
na Msemakweli Mwenyekiti wa Umoja wa Wainjilisti wa Kikristo nchini Tanzania
(UWAKITA) Mwinjilisti Samson Bulegi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kundi la Injili
kwa Wote ambalo moja ya shughuli zake ni kusahihisha upotoshaji wa imani ya
Kikristo unaofanywa na makundi ya Wahadhiri wa kiislamu, alisema vuguru za Zanzibar kwa sehemu kubwa
zina mkono wa dini na siasa.
Alisema
kisiasa JUMIKI na makundi mengine ya wanaharakati wa Kiislamu hayataki Muungano
kwa vile Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru wa kuabudu
ambao unakwamisha juhudi zao za kuunda dola la Kiislamu.
“Wanataka
muungano
uvunjike ili wapate fursa ya kueneza Uislamu na kuua Ukristo na ndio
maana hawawataki watu wa bara, huku pia wakichoma moto makanisa”,
alisema
Bulegi.
Alisema
kuwa Muungano unasababisha watu kutoka Bara kuingia kwa wingi Zanzibar kuhubiri Injii na kufungua makanisa;
hali inayosababisha Waislamu wengi kuokoka
na kuwa Wakristo,
“Unajua mambo ndivyo yalivyo. Hata Makamu wa
kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar Sheikh Maalim Seif
Sharif Hamad, aliwahi kukiri kwamba
Wakristo wanabaguliwa Zanzibar.
Mimi naiomba SMZ kukomesha jambo hili
kwani kila mtu ana haki ya kuishi kwa uhuru bila kubaguliwa”, alisema Bulegi.
“Bila kukomesha ubaguzi huu na unyanyasaji wa
Wakristo, moto utawaka na kusambaa kila mahali na hali kuwa mbaya zaidi”,
alitahadharisha Bulegi.
Labels:
Baraza la Makanisa ya Kipentekoste,
Kiislamu,
polisi,
Simbaulanga,
smz,
Zanzibar
Kauli ya Askofu Mtokambali kuhusu uchomaji wa makanisa Mbagala
KUHUSU
MATUKIO
YA
UCHOMAJI WA MAKANISA MBAGALA DAR ES SALAAM.
Oktoba
12 mwaka huu, matukio mabaya na yenye kutia doa sifa ya amani umoja na
Utengemano wa Taifa la Tanzania, yalijitokeza huko Mbagala Jijini Dar es
Salaam, wakati watu wenye jazba wanaoaminika kuwa ni Waislamu wenye msimamo
mkali walipovamia makanisa saba na kuyachoma moto eti kwa kulipiza kisasi cha
mtoto aliyekojolea kuran katika utani wa kitoto.
![]() |
| Askofu Mkuu wa TAG nchini Askofu Barnabas Mtokambali |
Katika
mkasa huo ambao ni kama muendelezo wa ghasia zingine zilizotokea kule Zanzibar
miezi michache iliyopita na kuteketeza makanisa mbalimbali mbali na kuharibu
mali za kanisa na zile za watu binafsi.Tukio
la Mbagala limesababisha makanisa saba kuharibiwa vibaya, mali kuibiwa na hata
kuhatarisha maisha ya watanzania na kuwafanya waishi kwa hofu na kupoteza
matumaini.
CHANZO
CHA TUKIO
Kwa
mujibu wa walioshuhudia, Polisi na wahusika (Waislamu) chanzo cha ghasia hizo
na mabishano ya kitoto baina ya watoto wa dini ya Kiislamu na kikristo,
waliobishana kuwa ikiwa mtu atakojolea kuran na kuitemea mate atageuka mbuzi au
nyoka.
Lakini
baada ya tukio hilo la kitoto watu walilikuza na kulipeleka kwenye misikiti na
hivyo kuchocheza ghasia. Kimsingi tukio lenyewe ni jepesi sana ukilinganisha na
matokeo yake. Ukweli kwamba waliofanya utani huo ni watoto na chanzo chake ni
mabishano ya kitoto, unatia shaka kuwa huenda kuna hoja nyuma ya pazia ambayo
isipotazamwa kwa makini inaweza kulete matokeo mabaya sana.
Jambo
linalonitia shaka ni kufanana kwa matukio ya kuchomwa moto kwa makanisa ya
Zanziabar na ya Mbagala ambapo hakukuwa na uhusiano wa vyanzo vya ghasia na
makanisa husika.
Mfano;
Ghasia za Zanzibar zilizopelekea kuangamizwa kwa makanisa zinaelezwa kuwa
zilitokana na kikundi cha Kiislamu cha Uamsho wa Mihadhara, kilichokuwa
kikiandamana kudai mjadala wa Muungano, lakini zikaishia kwenye uchomaji wa makanisa,
hapa hauonekani uhusiano wa kanisa na Muungano; nalazimika kujiuliza kulikoni?
Vivyo
hivyo tukio la Mbagala halina uhusiano wa moja kwa moja na kanisa kwa kuwa
hakuna ushahidi wala hata tetesi kuwa mtoto huyo alitumwa na kanisa lolote.
Wahusika wa dini ya Kiislamu akiwepo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
analielezea tukio la kitoto kama lisilostahili hata mtu kufunguliwa mashtaka
bali kuelekezwa tu. Ni vipi lisababishe uchomaji wa makanisa?
MAKANISA
YALIYOCHOMWA MOTO
Katika
ghasia hizo za aina yake, makanisa saba yamethibitishwa kuharibiwa kwa kuchomwa
moto, kupasuliwa vioo, viti na kuibiwa vyombo vya muziki na jenereta. Makanisa
hayo ni TAG Kizuiani, Agape, Kibonde maji, SDA Sabato, Mbagala Kizuiani,
Katoliki Kristo Mfalme Mbagala Rangi Tatu, Anglican Mbagala Kizuiani, KKKT,
Mbagala Zakhem na TAG, Shimo la Mchanga.
Pamoja
na majengo hayo kubomolewa kwa viwango tofauti mengine yakichomwa moto, pia
wahusika waliiba Genereta, na vyombo vya muziki vya makanisa hayo na kuvunja
magari na baadhi yao kuchomwa moto.
Choko
choko zilizinazoweza kuwa cahanzo cha matukio hayo ni:
Januari
sita mwaka huu, kikundi kimoja kinachoitwa JUAKITA, kiliitisha kongamano la
kujadili katiba mpya Tanzania, kwa upande wa Waislamu. Katika kongamano hilo
lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kulitolewas kauli
za kichozi kama:
1.
Lazima Rais ajaye atoke Zanzibar
2.
Kukabiliana na ukuaji wa kasi wa dini ya Kikristo
3.
Kupinga Muungano ili kuupa nguvu Uislamu
4.
Kupigana kufa na kupona kutetea maslahi yao wakati huu wa kuandaa katiba mpya.
Kauli
hizo zilitolewa na Sheikh Nasoro Mohamed, kutoka Zanzibar, ambaye alikuwa mgeni
rasmi. Baadaye zikaandaliwa kanda za CD zilizosambaza ujumbe huo.
Uchunguzi
unaonesha kuwa uchochezi huu umekuwa ukiwaandaa watu kusubiri vijitukio vidogo
tu ili kulipua ghasi. Tuliona jinsi makanisa yalivyochomwa kule Zanzibar. kwa
kuwakumbusha tu makanisan yaliyoangamizwa katika tukio hilo ni: EAGT, Elimu
Pentecost na TAG, Anglikana, Katoliki na FPCT.
Ni
jambo la kusikitisha kuwa matukio haya yanatokea siku mbili tu kabla ya
maadhimisho ya miaka 13, ya kifo cha Rais wa Kwanza, Mwl. Julius kambarege
Nyerere. Leo hotuba na midahalo inarindima kila mahali kumuenzi Nyerere, lakini
wengi wetu tukiwa tumejaa majozi baada ya nyumba zetu za ibada kuharibiwa
katika matukio yanayoashiri hatari kubwa.
Hofu
yangu ni kuwa, roho hii ya ubaguzi wa kidini ambayo Baba wa Taifa hayati Mwl.
Julius Kambarage Nyerere aliifananisha na dhambi ya kula nyama ya mtu, imekuwa
ikiyatafuna mataifa ya Afrika kama ifuatavyo:
1.
Mwaka 2000, vuguvugu la kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu (Sharia), lilianza
kwenye majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria, miaka michache baadaye majimbo kadhaa
yakajitangazia sheria hizo na tangu wakati huo kumekuwa na mapambano
yasiyoisha. Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka ya karibuni zaidi ya Wakristo
500 wameuawa kikatili na makanisa kuchomwa moto.
2.
Roho hii imekuwa ikienea kwa kasi katika maeneo mbali mbali ya Afrika ambapo
imelikumba taifa la Mali, majimbo ya kaskazini tayari yametangaza kujitenga na
kuna vuguvugu lenye kuhusisha mapigano ya silaha.
3.
Itakumbukwa kuwa miezi michache tu ilizopita vuguvugu hili la kudai utawala wa
kidini liliibuka nchini Kenya ambapo watu wanaojiita wanaharakati walianzisha
madai ya kutaka eneo la Pwani kujitenga na Jamhuri ya Kenya na kujitangazia
taifa la Kiislamu.
4.
Katika tukio hilo inasemekana mtoto huyo alitengenezewa mabishano ya kitoto
kuwa akichoma kurani atakuwa chizi naye akabisha
kisha
akapewa kiberiti na kurani akachoma tena walioandaa
mzaha
huo wakamkamata na kumpeleka mahakamani.
Tukio
linalofanana na hilo lilitokea tena Bagamoyo mkoani Pwani
ambapo
mtoto wa kike alishtakiwa na hata kuhukumiwa kifungo
kwa
madai ya kuchoma kuran lakini tukio lilikuwa katika mabishano
ya
midhaha ya kitoto
WITO
WANGU
Natoa
wito kwa Wakristo wote nchini kujiepusha na mizaha
inayoweza
kutengeneza sababu za kulipuka kwa ghasi na kutengeneza
mwanya
wa watu wenye nia mbaya kutekeleza agenda zao zaria Ili
kulinda
amani umoja na utengemano wetu, nawasihi viongozi wa makanisa
kuonya
na kukemea waumini na watoto wetu wasishiriki kwa namna yoyote ile mizaha
inayopelekea kuchoma au kuharibu vitabu au nyaraka
za
kidini.
Nawasihi
watanzania wote kwa ujula kujiepusha na mizaha ya kidini inayoweza kuchafua
amani yetu, na pale jambo lolote lenye kukera linapotokea tujiepushe kuwa
mawakala wa shetani wa kueneza chuki badala ya amani na upendo.
USHAURI
WANGU KWA SERIKALI NA VIONGOZI
Nawashauri
viongozi wa Serikali ambao leo wanatoa matamko na kushiriki midahalo ya
kumuenzi Mwl. Nyerere kukumbuka kuwa huyo alikuwa na mapenzi makubwa na amani
na umoja wa taifa. Kwa hiyo kumuenzi kwa vitendo ni kudumisha utawala bora,
unaofuata sheria usio na chembe ya ubaguzi wa aina yoyote.
Kulipuka
majukwaani kumuenzi Nyerere bila kuilinda na kuitetea amani ya nchi ni
kujidanganya.
Ni
wajibu wa kila Mtanzania kutii sheria na mamlaka kwa kuwa zimewekwa/kuruhusiwa
na Mungu, hivyo kuziasi ni Kumuasi Mungu, yaani ni dhambi. Hivyo kila Mtanzania
anastahili kukumbuka wajibu wake wa kutii mamlaka.
Viongozi
wenzangu wa dini wakumbuke kuwa wana wajibu mkubwa katika jamii, na jamii
inawasikiliza hivyo ni vyema wakawa makini katika matamshi na maelekezo yao ili
wasiwe chanzo cha kuchochea vurugu za kidini na uvunjaji wa amani.
Pia
ningependa kuwashauri viongozi wa serikali kusimama imara katika kusimamia
sheria na haki, na kuepuka kauli au vitendo vitakavyofanya baadhi ya watanzania
kudhani kuwa hawatendewi haki.
Ni
vema ieleweke kuwa matukio kama haya ya uvunjaji wa amani yasipodhibitiwa na
kukomeshwa haraka yanaweza kuumba chuki ambayo inaweza kuibua mlipuko mkubwa na
machungu kwa wananchi na matokeo yake yakawa mabaya kwa Taifa zima. Hekima na
busara inatufundisha kuwa tusipoziba ufa tutajenga ukuta.
Ni
vyema wenye dhamana ya kuongoza wakakumbuka kuwa wanawajibu mbele ya Mungu
aliyewaweka au kuwaruhusu kuingia madarakani na siku moja watatoa hesabu mbele
zake.
Ni
vyema viongozi wa Serikali wakajizuia kufanya maamuzi yanayoashiria upendeleo
kwa baadhi ya makundi ya kidini na kukiuka utawala wa sheria, mfano; kutii
waandamanaji na kuwaachia bila mashrti watu waliokamatwa kwa mujibu wa sheria
kuna jenga kiburi kwa makundi yenye kiu ya matumizi ya nguvu na kujenga hofu
kwa pande zingine.
Ni
vyema mamlaka zikasiamama katika sheria na kufanya hukumu kulingana sheria
badala ya kuamua mambo ya kisheria kisiasa.
WITO
MAALUMU KWA VIONGOZI WA DINI
Nitumie
nafasi hii kuwasihi vingozi wenzangu wa dini, kusimama imara katika kuombea
taifa na kuhubiri kwa nguvu ili kukabiliana na giza la kiroho ambalo linatishia
kuifunika nchi.
Takwimu
za karibuni kabisa za utafiti uliofanywa na taasisi ya Washnton DC iitwayo, Pew
Research Centre, na kurushwa na Televisheni ya CNN, Katika kipindi chake cha
Inside Africa, zilionesha kuwa watanzania asilimia 93, wanaamini mambo ya
ushirikina na uchawi wakati Uganda ni asilimia 29 na Kenya ni asilimia 27. Tu.
Mahali ambapo giza la kiroho limezingira kiasi hiki ni lazima matukio ya
kishetani yashamiri tuchukue hatua.
Mwisho,
natoa wito kwa watanzania wenzangu tuulinde umoja, amani na utengamano wa taifa
letu, tuikimbie dhambi ya ubaguzi kwa kuwa tukiiruhusu itatuangamiza sote.
Tuliombee taifa letu na kukiwa na mbegu ya chuki tuimalize kwa njia ya
majadiliano na vikao vya pamoja vinavyohusisha viongozi wa dini zote na
serikali pia.
Imetolewa
leo 14/10/2012
Na
Dk. Barnabas Mtokambali
Askofu
Mkuu wa TAG
Labels:
News,
Nukuu za Watumishi
Sunday, 14 October 2012
UCHOMAJI MAKANISA MBAGALA
Ndugu msomaji
Shalom
Kumetokea tukio la ajabu na mbalo sasa linakuwa kawaida ka nchi yetu juu ya uchomaji makanisa, kabla jeraha la Zanzibar halijapoa makanisa mbagala matatu yamechomwa Mbagala. Sababu ikiwa ni mabishano ya watoto kwamba ukikojolea kuran atageuka Panya au paka, MTOTO (MKRISTO) naamini akisukumwa na imani akaamni kuwa hawezi kugeuka panya kwa kukojolea kuran na hivyo akaamua kuthibitisha kwa kukojolea kuran na kama alivyoamni hakugeuka panya (MTOTO SHUJAA) Kwa sababu akawa amefichua uongo mkubwa kwamba kuran ina uwezo wa kumgeuza mtu panya wakaksirika na kutaka kujichukulia sheria mkononi wamuue lakini kakimbilia Kituo cha Polisi, kwa hasira wakakimbia kuchoma makanisa. Hatuwezi kusema nchi ina amani wakati makanisa yanaendelea kuchomwa moto, hatuwezi kusema nchi haiamni dini wakati dini fulani imekuwa ikituma mabavu kuinyanyasa dini nyingine kwa kuchoma makanisa. Kuchoma makanisa kuna athari mbaya kwa mkristo kwani sasa atashiriki ibada kwa wasi wasi na hata mazungyumzo baina ya muislamu na mkristo yameingia dosari. Chonde kwa serikali kuhakiksha inawadhibiti hao wenye kuwa na chuki na ukristo.
IMANI THABITI ITADUMU MILELE HATA MASINAGOGI YAKICHOMWA, TUTENDELEA KUYANENA TUNAYOYAAMINI

Mawe yametoboa vioo vingi
Katika madhabahu,pameharibiwa

Mabenchi yamepinduliwa na kuvunjwa
Mimbari imechomwa na kuharibiwa



Ofisi ya Kanisa imechomwa moto
Wachungaji wa kanisa hili wakisubiria taarifa kutoka polisi
Hawa wanafanya maombi na nimesikia wakiwaombea waislamu mungu awasamehe
Vifaa vya uimbaji vimechomwa moto
Washarika wakiwa kanisani kwao asubuhi hii
Gari la mchungaji pia limeharibiwa kabisa

Shalom
Kumetokea tukio la ajabu na mbalo sasa linakuwa kawaida ka nchi yetu juu ya uchomaji makanisa, kabla jeraha la Zanzibar halijapoa makanisa mbagala matatu yamechomwa Mbagala. Sababu ikiwa ni mabishano ya watoto kwamba ukikojolea kuran atageuka Panya au paka, MTOTO (MKRISTO) naamini akisukumwa na imani akaamni kuwa hawezi kugeuka panya kwa kukojolea kuran na hivyo akaamua kuthibitisha kwa kukojolea kuran na kama alivyoamni hakugeuka panya (MTOTO SHUJAA) Kwa sababu akawa amefichua uongo mkubwa kwamba kuran ina uwezo wa kumgeuza mtu panya wakaksirika na kutaka kujichukulia sheria mkononi wamuue lakini kakimbilia Kituo cha Polisi, kwa hasira wakakimbia kuchoma makanisa. Hatuwezi kusema nchi ina amani wakati makanisa yanaendelea kuchomwa moto, hatuwezi kusema nchi haiamni dini wakati dini fulani imekuwa ikituma mabavu kuinyanyasa dini nyingine kwa kuchoma makanisa. Kuchoma makanisa kuna athari mbaya kwa mkristo kwani sasa atashiriki ibada kwa wasi wasi na hata mazungyumzo baina ya muislamu na mkristo yameingia dosari. Chonde kwa serikali kuhakiksha inawadhibiti hao wenye kuwa na chuki na ukristo.
IMANI THABITI ITADUMU MILELE HATA MASINAGOGI YAKICHOMWA, TUTENDELEA KUYANENA TUNAYOYAAMINI
Hapa nimechapisha picha za matukio ya uchomaji makanisa mbagala na ziara ya Mhe. Raisi kwa mujibu wa blogu mbalimbali kama zilivyochapishwa chini ya kila habari au picha.
RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA MAKANISA YALIYOCHOMWA NA WAISLAM MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM
Posted by PASTOR
GORDON KALULUNGA
Rais Kikwete atembelea Makanisa yaliyochomwa moto na kuharibiwa Mbagala jijini Dar es Salaam
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, akiangalia uharibifu mkubwa uliofanywa katika
kanisa la Pentekoste la Mbagala, jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu
za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari za mtoto mmoja wa sehemu
hiyo, kukojolea Msahafu wa Kuraan Tukufu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi, uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu za Waislamu, Ijumaa iliyopita kufuatia habari za mtoto mmoja wa sehemu hiyo, kuukojolea Msahafu wa Kuraan Tukufu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye magari yaliyokuwa yameegeshwa ndani ya kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu za Waislamu, Ijumaa iliyopita kufuatia habari za mtoto mmoja wa sehemu hiyo, kuukojolea Msahafu wa Kuraan Tukufu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam Bw. M Mkosimonga uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo, huko Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu za Waislamu, Ijumaa iliyopita kufuatia habari za mtoto mmoja wa sehemu hiyo, kuukojolea Msahafu wa Kuraan Tukufu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa baadhi ya waumini wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam kufuatia uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo, huko Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu za Waislamu, Ijumaa iliyopita kufuatia habari za mtoto mmoja wa sehemu hiyo, kuukojolea Msahafu wa Kuraan Tukufu.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana
Dayosisi ya Dar es salaam Bw. M Mkosimonga uharibifu mkubwa uliofanywa
kwenye kanisa hilo, huko Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu
za Waislamu, Ijumaa iliyopita kufuatia habari za mtoto mmoja wa sehemu
hiyo, kuukojolea Msahafu wa Kuraan Tukufu.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Askofu Msaidizi wa Kanisa la
Kiinjili la Kirutheli Dayosisi ya Dar es salaam na Pwani Mkosimonga
uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo, huko Mbagala
jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu za Waislamu, Ijumaa iliyopita
kufuatia habari za mtoto mmoja wa sehemu hiyo, kuukojolea Msahafu wa
Kuraan Tukufu.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Askofu Msaidizi wa Kanisa la
Kiinjili la Kirutheli Dayosisi ya Dar es salaam na Pwani Mkosimonga
uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo, huko Mbagala jijini Dar
es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari
kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana
Dayosisi ya Dar es salaam Bw. M Mkosimonga uharibifu mkubwa uliofanywa
kwenye kanisa hilo, huko Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu
za Waislamu, Ijumaa iliyopita kufuatia habari za mtoto mmoja wa sehemu
hiyo, kuukojolea Msahafu wa Kuraan Tukufu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi, uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu za Waislamu, Ijumaa iliyopita kufuatia habari za mtoto mmoja wa sehemu hiyo, kuukojolea Msahafu wa Kuraan Tukufu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye magari yaliyokuwa yameegeshwa ndani ya kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu za Waislamu, Ijumaa iliyopita kufuatia habari za mtoto mmoja wa sehemu hiyo, kuukojolea Msahafu wa Kuraan Tukufu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam Bw. M Mkosimonga uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo, huko Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu za Waislamu, Ijumaa iliyopita kufuatia habari za mtoto mmoja wa sehemu hiyo, kuukojolea Msahafu wa Kuraan Tukufu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa baadhi ya waumini wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam kufuatia uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo, huko Mbagala jijini Dar es Salaam wakati wa vurugu za Waislamu, Ijumaa iliyopita kufuatia habari za mtoto mmoja wa sehemu hiyo, kuukojolea Msahafu wa Kuraan Tukufu.
Na mwandishi wetu
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, ametoa pole kwa waumini wa makanisa yaliyochomwa moto na kuharibiwa
katika eneo la Mbagala, Dar es Salaam, akisisitiza kuwa wote
waliohusika katika vurumai hizo na uharibifu huo na wale waliowatuma
watashughulikiwa ipasavyo na Serikali.
Aidha,
Rais Kikwete ameyaelezea matukio ya jana, Ijumaa, Oktoba 12, 2012 kuwa
ni ya aibu na fedheha ambayo halikustahili kutokea katika nchi yenye
historia ya miaka mingi na ya kutukuka ya waumini wa dini mbali mbali
kuvumiliana na kuishi kwa amani.
Rais
Kikwete pia ametoa wito kwa viongozi wa dini zote mbili kuwa watulivu
katika hali ya sasa na kutokuhamanika na kuviachia vyombo vya Serikali
kufanya kazi, akiwaasa viongozi wa makanisa yaliyoharibiwa kuwa watulivu
na kutokufikiria hatua za kulipiza kisasi kwa sababu kamwe hatakuwepo
mshindi katika vurumai hasa ya kidini.
Rais
Kikwete ameyasema hayo leo, Jumamosi,Oktoba 13, 2012, wakati alipofanya
ziara ya ghafla kutembelea makanisa yaliyochomwa moto katika eneo la
Mbagala kufuatia vurumai za jana ambako chanzo chake ni mtoto kukojolea
Kitabu Kitukufu cha Qoran katika eneo hilo hilo la Mbagala.
Rais
Kikwete ametembelea makanisa matatu ambako alishuhudia yalivyoharibiwa
kwa vioo vya madirisha kuvunjwa, madhabau kuharibiwa na biblia kuchomwa
moto, vyombo vya muziki kuibwa ama kuvunjwa, magari ya viongozi wa dini
na waumini kuchomwa moto, vioo vya magari hayo kuvunjwa na mali za ndani
ya magari, zikiwamo redio kuibiwa, nguo za wachungaji na hata divai
kuibiwa.
Rais
Kikwete ameanzia ziara yake kwenye Kanisa la Mbagala kwa Yesu la
Tanzania Assemblies of God (TAG) ambako amepokelewa na Askofu Dkt.
Magnus Muhiche na kuonyeshwa uharibifu mkubwa uliofanyika kwenye kabisa
hilo ambalo limeonekana kufanyiwa uharibifu mkubwa zaidi kuliko makanisa
mengine ikiwa ni pamoja na jenereta ya umeme ya kanisa kuibiwa.
Katika
ziara hiyo ambako Rais Kikwete ameandamana na Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mheshimiwa William Nchimbi aliambiwa na Kamanda wa Mkoa Maalum
wa Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova kuwa mpaka sasa watu 122
wametiwa mbaroni kufuatia vurumai na fujo za jana.
Kati
ya hao, watu 36 wamekamatwa kwa kufanya uharibifu kwenye makanisa hayo
na wengine 86 wamekamtwa kwa kufanya fujo za kawaida na za jumla katika
hali ya mazingira ya jana.
Rais
amesema kuwa ni kweli kuwa kitendo cha mtoto kukojolea Qoran ni kitendo
cha makosa lakini vile vile kuvunja makanisa nalo ni kosa hasa kwa
kutilia maanani kuwa uharibifu wa kukojolea Qoran ulikuwa tayari
unashughulikiwa na vyombo vya ulinzi na usalama wakati makanisa yanaanza
kuchomwa.
“Katika
hali hiyo basi nawaomba viongozi wa pande zote mbili wawe wavumilivu na
wasihamanike kwa sababu mazingira ya sasa ndiyo kipimo cha uongozi na
kiongozi akihamanika basi wafuasi wake watahamanika mara 10 zaidi.
Waiachie Serikali na vyombo vyake kulishughulikia jambo hili,” amesema
Rais Kikwete na kuongeza:
“Kwenye
vurumai za kidini hakuna mshindi. Ni shughuli haina tija. Nawaombeni
viongozi kuhakikisha kuwa jambo hili haliigawi jamii yetu ambayo kwa
miaka mingi imeishi pamoja bila kujali tofauti zao za kidini. Linalofaa
kwa sasa ni viongozi wa pande zote kukaa pamoja na kuzungumza namna ya
kurejea utulivu, amani na mshikamano.”
Rais
Kikwete pia ametembelea Kanisa la Utatu Mtakatifu la Madhehebu ya
Anglikana ambako amepokewa na Katibu wa Kanisa hilo, Bwana Albert
Mukasimongwa ambaye vile vile amemwonyesha uharibu uliofanywa kwenye
Kanisa hilo wakati wa fujo hizo ikiwa pamoja na kuharibu kabisa
madhabau.
Rais
amemalizia ziara yake kwenye Kanisa la KKKT ambako ameshuhudia kundi
kubwa la waumini wakiendelea kusali, kuimba na kulia. Kwenye Kanisa hilo
amepokelewa na Mchungaji George Fupe ambaye pia ni Msaidizi wa Askofu
wa Jimbo la Dar es Salaam la KKKT aliyewaomba waumini “kutulia na
kusikiliza Sauti ya Faraja ya Mheshimiwa Rais.”
Rais
amewaambia waumini hao: ‘Jamani poleni sana. Nimekuja kuwapeni poleni
kuhusu jambo hilo la kusikitisha, jambo la fedheha, jambo la aibu
kabisa, jambo ambalo hatukutegemea litokee katika nchi yenye historia
nzuri sana ya uvumilivu wa kidini.
Ameongeza
Rais Kikwete: “Ombi langu kwa pande zote ni tulivu tukiongozwa na
viongozi wetu. Tusilipize kisasi kwa sababu hilo halitasaidia. Tuviachie
vyombo vya sheria vifanye kazi yake. Nawahakikishi eni kuwa yoyote
aliyehusika atashughulikiwa ipasavyo na pamoja wale waliowatuma. Nao
hawataachiwa.”
Subscribe to:
Posts (Atom)

















